Serikali kurejesha matumizi ya kadi kwa abiria mabasi ya Mwendokasi

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameagiza kuanzia Julai Mosi mwaka huu, kuanza uhakiki wa tiketi za kielektroniki katika usafiri wa mabasi yaendayo kwa haraka kwa kutumia mfumo wa posi ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Amesema kuwa utekelezaji wa hilo ni hatua za awali wakati unasubiriwa mfumo mkubwa utakaohuisha matumizi ya kadi na mageti ambao ndio utakaokuwa ni suluhu ya kudumu.

Waziri Ummy ametaka uhakiki huo wa kutumia posi kuanza haraka wakati mfumo mkubwa unaotarajiwa kutekelezwa Novemba mwaka huu, unasubiriwa ili kuepuka udanganyifu, wizi na upotevu wa mapato.

“Nataka mapema tuwe tumekomesha utoaji wa tiketi zisizohakikiwa, hapa tunaruhusu wizi kufanywa watu wanakuwa na vitabu vyao vya tiketi, Rais Samia na Waziri Mkuu waliyasema haya,” amesema Waziri Ummy.

Ameendelea kusema kuwa matumizi ya tiketi hizo kunapelekea kujitokeza kwa udanganyifu na wizi wa mapato kutokana na baadhi ya watendaji wasio waaminifu kuingiza sokoni tiketi zao na kusisitiza kuwa lazima kuwepo kwa utaratibu unaohakikisha tiketi zinatolewa moja kwa moja katika mashine na kumfikia abiria wakati huo.
 
Serikali watairudisha ila baadae wapigaji wataharibu mifumo yake ili mambo yao yaende sawa.
 
Ajiri wachina watengeneze waweke hio mifumo inayotumika kwenye mabasi kama hayo kwao, na tren pia, wabongo longolongo nyingi
Mfumo upo mzuri kabisa wameuzima ili waweze kufanya upigaji.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameagiza kuanzia Julai Mosi mwaka huu, kuanza uhakiki wa tiketi za kielektroniki katika usafiri wa mabasi yaendayo kwa haraka kwa kutumia mfumo wa posi ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Amesema kuwa utekelezaji wa hilo ni hatua za awali wakati unasubiriwa mfumo mkubwa utakaohuisha matumizi ya kadi na mageti ambao ndio utakaokuwa ni suluhu ya kudumu.

Waziri Ummy ametaka uhakiki huo wa kutumia posi kuanza haraka wakati mfumo mkubwa unaotarajiwa kutekelezwa Novemba mwaka huu, unasubiriwa ili kuepuka udanganyifu, wizi na upotevu wa mapato.

“Nataka mapema tuwe tumekomesha utoaji wa tiketi zisizohakikiwa, hapa tunaruhusu wizi kufanywa watu wanakuwa na vitabu vyao vya tiketi, Rais Samia na Waziri Mkuu waliyasema haya,” amesema Waziri Ummy.

Ameendelea kusema kuwa matumizi ya tiketi hizo kunapelekea kujitokeza kwa udanganyifu na wizi wa mapato kutokana na baadhi ya watendaji wasio waaminifu kuingiza sokoni tiketi zao na kusisitiza kuwa lazima kuwepo kwa utaratibu unaohakikisha tiketi zinatolewa moja kwa moja katika mashine na kumfikia abiria wakati huo.
Ninashauri kuwepo na waziri wa kushughukika na Jiji la dar es salaam tu,kama ilivyo Nairobi. Sasa dada yetu Ummy mwalimu mtampasua mshipa wa kichwani. Mmempa wajibu wa kila kitu mwisho utendaji wake hautaonekana.wakati tunakua ni jembe.
 
Kiukweli walipotosha na kukwepa kutumia kard ilikuwa dhahiri walipanga kupiga...

Walikwepa kabisa..... ⛴️ Ferry kigamboni wanakula sana kwa style hii
Ukiona chini wanaiba, wizi umenzia huko juu, Kuendesha haya mashirika ni rahisi sana, ila wizi ndio kansa inatafuna hizi taasisi
 
Nakubaliana..maana wizara ya fedha wanajiandikia malipo Kazi Maalum, sijui honoraria, kuandaa, kumpigia nk yaani Mh Rais aangalie kila kona atakuta uwozo huu...Kuna watendaji wanafanya wenzao waishi kishetani.
 
  • Thanks
Reactions: Lob
Sio vibaya tukatafuta likampuni toka ngambo lenye uzowefu wa muda mrefu wa mambo haya ya tiketi (ushauri + uendeshaji) NDIO SULUHISHO WATANZANIA WATAHARIBU TU I don't trust them hata umuone anaheshima kiasi gani.
HATA SISI WENYE MADALADALA TUNAHITAJI MASHINE ZA TIKETI
#Mwigulu.
 
Back
Top Bottom