Serikali Kushirikisha Vijana Kupambana na Uhalifu, Bashungwa Atoa Onyo Kali

Serikali Kushirikisha Vijana Kupambana na Uhalifu, Bashungwa Atoa Onyo Kali

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Wizara kupitia vyombo vya usalama na taasisi nyingine za Serikali zitashirikiana na Vijana ili kupata suluhu kwa baadhi ya changamoto zilizopo na zinazoendelea kujitokeza katika jamii ikiwa ni pamoja uhalifu, kupambana rushwa, dawa za kulevya na Unyanyasaji wa kijinsia.​

Waziri Bashungwa ameyasema hayo leo Disemba 14, 2024, wakati akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Skauti Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni, jijini Dodoma.

"Tuna nia ya dhati kushirikiana na Vijana wa Skauti katika kushughulikia masuala ya kihalifu, nina amini kabisa kupitia jukwaa hili tutaweza kwenda kwa jamii kupitia mafunzo na utimamu mlio nao kuifanya nchi izidi kuwa bora ya amani na usalama” amesema Bashungwa.

Hata hivyo, Waziri Bashungwa amesisitiza umuhimu wa vijana wa skauti katika kutunza maadili ya Nchi na kuhamasisha vijana wengine kutokuingia kwenye vitendo vya uvunjaji wa sheria vinavyoharibu muelekeo wa maisha yao.

"kijana ukiingia kwenye dawa za kulevya unapoteza muelekeo na sisi hatufurahii kuona kijana anapoteza muelekeo na kuvunja sheria ya nchi kwahiyo tunajukumu kubwa la kuwasaidia" amesisitiza.

Aidha, Amesema Wizara kupitia Vyombo vyake vya Usalama ina programu mbalimbali ambazo vijana wakishirikishwa itasaidia jamii iwe salama pamoja na mali zao.

Naye, Rais wa Chama cha Skauti Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda amesema kazi kubwa ya skauti ni kukuza na kulinda maadili ya Mtanzania, kuendeleza ujasiri hasa kwa vijana kujishughulisha na shughuli za maendeleo kwa jamii.

Kwa Upande wake, Skauti Mkuu wa Tanzania, Rashid Kassim Mchata amesema dhumuni la Mkutano huu ni kupitisha rasimu ya mabadiliko ya Katiba ya chama ili kukidhi mahitaji ya sasa na kupitisha sera mbalimbali za chama.

WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.27.52.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.27.54.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.27.56.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.27.57.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.27.59.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.28.01.jpeg
WhatsApp Image 2024-12-14 at 16.28.03.jpeg
 
Mbona salute imepigwa huku kifole kimewekwa mkunjio wa 0?
 
Kijana wangu huko shuleni akijunga Skout,...siku nikajua , ataambulia fimbo nyingi sana,...🚮🚮
 
Kijana wangu huko shuleni akijunga Skout,...siku nikajua , ataambulia fimbo nyingi sana,...🚮🚮
Unakosea sana Mkuu, skauti ni chama bora kwa vijana wadogo. Japo changamoto zipo hasa kipindi hichi na yanakabiliwa kwa haraka.
 
Mgambo wako mbali kimafunzo kuliko scout. Hao ni kaka ceremonial wanna be troops
Watu wengi hawajui kuwa Mgambo ni kamandi ya jeshi na pia hawajui kuwa skauti ni chama kinacholea vijana na sio kikundi cha kijeshi.
 
Unakosea sana Mkuu, skauti ni chama bora kwa vijana wadogo. Japo changamoto zipo hasa kipindi hichi na yanakabiliwa kwa haraka.
Ni UPUUZI tu,.... mtoto anakuwa busy for nothing,......na nimezuia wengi kujiunga huko,........hakika wangu atauona moto siku nikibaini yupo huko......
 
Ni UPUUZI tu,.... mtoto anakuwa busy for nothing,......na nimezuia wengi kujiunga huko,........hakika wangu atauona moto siku nikibaini yupo huko......
Sikushangai sana Mkuu, ni tatizo la kutokufahamu mambo tu na kuwa mbinafsi.
 
Sikushangai sana Mkuu, ni tatizo la kutokufahamu mambo tu na kuwa mbinafsi.
Endeeleni kuwaacha WATOTO wenu watumike kwenye mbio za mwenge kama toilet paper,...huku wao wakijiita makomando
 
Sasa waanze kuwalipa maskauti pia
Kiongozi anayependa kuabudiwa kwa kupewa heshima kama hizi anaonyesha akili zake zilivyo ndogo. BTW Tanzania ni nchi ya matamko ya wanasiasa na haya yote aliyosema ni matamko kama mengine yaliyokwishatolewa. Ulaya kamwe huwezi kusikia matamko ya wanasiasa yakiandamana namna hii bali utaona utendaji
 
Endeeleni kuwaacha WATOTO wenu watumike kwenye mbio za mwenge kama toilet paper,...huku wao wakijiita makomando
Acha watoto waishi wakati wao kiongozi ili baadae wasikuone baba mchoyo.
 
Naomba kujua maana yake afande
Hivyo vidole vitatu vilivyosimama vinamaanisha au kumkumbusha skauti mambo matatu
1. WAJIBU KWA MUNGU Nna TAIFA LAKE
2. WAJIBU KWA WATU WENGINE
3. WAJIBU KWA NAFSI YAKE

Hivyo viwili vilivyokunjwa vinamkumbusha skauti mambo haya;
4. UNDUGU/UMOJA WA MASKAUTI
5. MAFUNZO YA UTAIFA na TABIA

Yote hayo ni kumfanya kijana awe bora wakuigwa na kutegemewa na Taifa na Jamii yake.

Ni mafunzo mazuri sana hasa yakitolewa ipasavyo. Kuna mambo mafunzo kijana atafaidika nayo kwenye maisha yake ukubwani.
 
Acha watoto waishi wakati wao kiongozi ili baadae wasikuone baba mchoyo.
Waache wa kwako mkuu,.... watoto wangu wana uhuru wote wa kuchagua chochote kile kizuri lakini sio UPUMBAVU,...USKOUT shuleni ni UPUMBAVU.... watoto wa maskini ndo unawakuta na huu ujinga,...nenda shule zinazojielewa uone kama wana huu UZWAZWA,..
 
Back
Top Bottom