Serikali kutoa Elimu na kuwapa ujuzi watu wenye Ulemavu wanaoonekana wakiombaomba na wanaotumiwa kama chombo katika kuomba

Serikali kutoa Elimu na kuwapa ujuzi watu wenye Ulemavu wanaoonekana wakiombaomba na wanaotumiwa kama chombo katika kuomba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Esther Edwin Malleko ameiuliza swali Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu "Watu wenye ulemavu wameonekana wakiwa ombaomba na kutumiwa kama chambo katika kuomba, ni mkakati upi wa Serikali katika kuwasaidia watu hawa kujikwamua kiuchumi?"

Swali la Mhe. Esther Malleko lilijibiwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi kwa niaba ya Waziri Mkuu ambapo alijibu Mikakati ya Serikali ya Awamu sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na Utekelezaji wa Mipango ifuatayo;

1. Kutoa Elimu ili kubadili mitazamo hasi kuwa chanya (Disability is not Inability), imefungua Vyuo vya Ufundi Stadi na Huduma za Utengamao kwa Watu wenye ulemavu zaidi ya Saba (Dar es alaam, Tanga Mwanza Singida, Mtwara, Tabora) sambamba na Inclussive education kuendelea.

2. Serikali imeendelea kuwapa Mikopo ya 2% ya mapato kutoka fungu la asilimia 10% ya mapato wezeshi ya kila Halmashauri pamoja na mifuko mingine ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

3. Serikali inaendelea kutoa Elimu ya Ujasiliamali na ufunguzi na fursa za Mikopo, Ajira na Mitaji.

4. Kutoa Miongozo Mbalimbali ya Utambuzi wa watu wenye ulemavu, Mfuko wao Maalum, pamoja Uratibu na tathimini.

5. Kwa Maagizo ya Upendo na haki ya Mhe. Rais Dkt. Samia na Maelekezo ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu tayari tumeanza kuhakikisha Ajira zote zinazotoka 3% kwa mujibu wa Mwongozo wapewe watu wenye Ulemavu na pia kuendeleza makubaliano na Wizara husika kupata Punguzo na nafuu za Kodi au kuondoa kodi kwa Vifaa saidizi kwa Watu Wenye Ulemavu ikiwemo Mafuta, Vitimwendo, fimbo Nyeupe.

6. Serikali inaendelea kushawishi na kuwasaidia Watu wenye Ulemavu Wajiunge katika Vyama kuwa na Jukwaa au Shirikisho moja ili kuirahisishia zaidi Serikali Kukutana nao, kupokea agenda na matakwa yao na kuyatafutia Ufumbuzi kwa makubaliano ya pamoja na kwa mujibu wa sheria.

"Mikakati hiyo baadhi inalenga kuwainua na kuwakwamua Kiuchumi, na kimaarifa na ujuzi ili wasiwe tegemezi na kuepukana na kuombaomba, ni rai yangu pia Jamii yote tuwe msaada kwao kuwategemeza." - Mhe. Katambi
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-04-27 at 10.17.58.mp4
    12.7 MB
Hii haitoshi kwa sasa hakuna sehemu ambapo 03% ya wafanyakazi wanaoajiriwa wana ulemavu hamna!!!! Nitajie taasisi au hata sehemu tu moja! Hamna ni maneno tu maneno tu na sis hata tunachoka!
 
Back
Top Bottom