Serikali kutumia bilioni 500 kujenga vituo vya kupoozea umeme

Serikali kutumia bilioni 500 kujenga vituo vya kupoozea umeme

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Katika bajeti ya mwaka huu Serikali imetenge Shilingi bilioni 500 ambazo kupitia mradi wa Gridi Imara itajenga vituo vya kupooza umeme katika maeneo 13. nchini.

"Kwenye maeneo yenye shida zaidi, tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita imetoa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa gridi kwenye maeneo yanye matatizo makub-wa," alisema Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato.

Pia alisema katika kipindi cha miaka sita ijayo, wizara hiyo inakusudia kujenga vituo vya kupooza umeme katika kila wilaya nchini.

Byabato alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Makete, Festo Sanga (CCM). Sanga (CCM) alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi ya kubadilisha laini ya umeme unaokwenda Makete badala ya kutumia inayotoka Mbeya ambayo inasumbua, imechoka na umeme unakatika katika mara kwa mara. Byabato alijibu mojawapo ya changamoto ya umeme ni kusafirishwa umbali mrefu kutoka kwenye chanzo.

Alieleza kuwa tathmini ilifanyika kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na wakabaini kwamba kuna makundi matatu ya watu wana shida zaidi, shida za kati na wengine maisha yanaweza kuendelea na ndiyo maana serikali imetoa fedha kusaidia maeneo yenye shida kubwa.​
 
Wajenge na vya kupoooza..Ndio maana hilo shirika linaendeshwa kwa hasara
 
Back
Top Bottom