Serikali kutumia Tsh. Bilioni 35.1 kununua Magari 316 ya Wagonjwa

Serikali kutumia Tsh. Bilioni 35.1 kununua Magari 316 ya Wagonjwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, Serikali imetenga shilingi Bilioni 35.1 kwa ajili ya ununuzi wa magari 316 ya kubeba wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Dkt. Dugange amesema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini, David Kihenzile aliyetaka kujua ni lini Serikali itapeleka magari ya kubeba wagonjwa katika vituo vya afya vya Mtwango na Mgololo.

Amesema taratibu za manunuzi zinaendelea na magari hayo yatagawiwa kwenye halmashauri zote 184 nchini, ikiwemo halmashauri ya wilaya ya Mufindi ambayo itapewa magari mawili ya kubeba wagonjwa.

Naibu Waziri huyo Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema, Serikali inatambua umuhimu na uhitaji wa magari ya kubeba wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

BUNGENI DODOMA
 
Back
Top Bottom