Amani iwe nanyi, tetesi nilisozipata zinatabiri kwamba Serikali imeshaunda task force kuchunguza na kubaini wahusika wa vitendo vya utekaji na utesaji dhidi ya raia na huenda ikaundwa tume huru ya kimahakama kuchunguza shambulio la Dodoma dhidi ya Lissu.
Kwa ushahidi wa mazingira kupitia vyanzo vya habari kama magazeti na mitandao ya kijamii ndugu Tundu Lissu ana mgogoro wa malumbano na wapinzani watatu ambao ni,
1. Mgogoro na wawekezaji wote tu mashahidi.
2. Mgogoro na serikali kwani amekuwa mkosoaji mkuu
3. Mgogoro na maadui ndani ya chama hasa kuelekea mbio za urais 2020.
Kwa mazingira haya ni vigumu sana kubashiri ni nani hasa alitaka kumuua ndugu Tundu Lissu.
Nawasihi tuwe wavumilivu na wenye subra tuache ushabiki na ukada kwa suala linalohusu maisha ya mtu.
Mwisho naona kama kweli serikali itaunda tume ya kimahakama inaweza kuleta mwarobaini dhidi ya vitendo vya kidhalimu vinavyoota mizizi kila kukicha, hatujui kesho itatokea kwa nani.
Mungu ibariki Tanzania