Wewe nadhani kuna kitu unapungukiwa.
Lisu ana mgogoro gani na chama? Unabwabwaja kuhusu Zito, huku huelewi unachoongea.
Zito aliingia kwenye mgogoro kwanza kwa kukisaliti chama. Kufanya vikao na maofisa wa CCM na serikali bila ya taarifa yoyote kwa chama kipindi cha kampeni. Hakumfanya kampeni mgombea wa Urais wa chama. Alikuwa akifanya vikao na mawasiliano mengi na watu ambao ni maadui wa chama, na hakuweza kueleza vikao hivyo vilikuwa vinahusu nini?
Zito aliamua kwenda kinyume cha maamuzi ya chama yaliyokuwa yamefanywa kwenye vikao. Wakati chama kilipoamua kuwa hakimtambui JK, yeye aliamua kumtambua.
Baadaye akafanya harakati za chini kwa chini nje ya utaratibu wa chama, kutaka kupindua uongozi wa chama. Pamoja na hayo yote, chama kilimivumilia. Hata kilipoamua kufanya kikao juu ya kuamua hatima yake, aliamua kujiuzulu mwenyewe.
Hata baada ya kujiuzulu, nani alimdhuru Zito. Kuna wehu wa chama chenu wakaanza kutengeneza hadithi eti Zito amewekewa sumu lakini aliwaumbua alipokataa kuwa hakuwekewa sumu. Na hiyo ilitokana na akili ndogo za wana-Lumumba kutokuelewa maana ya food poisoning wakatafsiri kuwa aliwekewa sumu kwenye chakula. Tatizo la ujinga, ambalo hata TWAWEZA limigundua kuhusiana na wapenzi/wafuasi wa CCM (wengi wao ni wale wenye elimu na uelewa mdogo).