Serikali kuwabana zaidi waagizaji Magari yaliyotumika ili kulinda uzalishaji wa ndani

Hakika nimeshtushwa na Taarifa ya Serikali kuwa inataka kubana zaidi USHURU kwa Magari yaliyotumika (USED) ili Masikini Watanzania WASHINDWE KABISA kununua hayo Magari ETI wanunue MAGARI MAPYA ambayo kuna MWEKEZAJI Katoa Sh BIL. 1O ili kuanzisha Kiwanda cha MAGARI MAPYA.

Najiuliza ni Watanzania Wangapi wenye Uwezo wa kununua MAGARI MAPYA? Kama hata Mawaziri na Wabunge wetu nao kimbilio lao ni haya haya Magari Yaliyotumika (Used) Mwananchi gani atanunua GARI JIPYA?
USHAURI kwa Serikali.

Badala ya Kumlinda Huyo Mwekezaji Serikali iwaangalie Wananchi wake kwa kupunguza USHURU badala ya kuuongeza ili Masikini Wananchi Waweze kununua MAGARI YALIYOTUMIKA kwa wingi ila irekebishe Umri wa Gari toka Limetengenezwa ili kubana kuingiza Magari ya muda mrefu toka yametengenezwa.
 
Ndo maana mimi naikubali sana Zambia
 
Mfano mzuri tu ziangalie hizo eicher zao
 
Mkuu mtanunua tu mahindra mpya ina cc 800 ukubwa wa duet na itauzwa kati ya mil 5 hadi 6 .milage 0
Dunia inahamia kwenye electric vehicles, kampuni nyingi za magari duniani zimetangaza kufikia 2030 wanaacha kabisa kutoa hizi combustion engines, engine zinazotumia mafuta, China sasa hivi inatoa gari za umeme kwa kasi ya ajabu, sasa hizo mahindra za cc 800 ni kituko tu.
 
mkuu mpaka leo huku tunatamba na harrier za 2004 ukiwa na ya 2010 tunasimama ukiingia baa.sisi hayo ya umeme ni after 40 yrs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…