Serikali kuwabana zaidi waagizaji Magari yaliyotumika ili kulinda uzalishaji wa ndani

Serikali kuwabana zaidi waagizaji Magari yaliyotumika ili kulinda uzalishaji wa ndani

Mahindra sio gari za kusema wabane Kampuni used kama Land Cruiser,Ford Ranger na Nissan wao wawaruhusu kuja kushindana na si kufanya kama Mwendokasi harafu baadae wakaferi Nchi yenyewe haina magari ya kutosha zaidi ya hizo V 8 za kodi harafu mnataka Wananchi waendelee kubanana kwenye Bus...
 
Watanzania wajiandae kuanza kununua magari mapya baada ya serikali kukamilisha kuandaa sera mpya ambayo itapiga marufuku Watanzania kununua magari yaliyotumika.

Sera hii mpya inaungwa mkono na wawekezaji ambao watakuwa na jukumu la kuingiza magari mapya na pia kushirikiana na makampuni ya kigeni yanayounda magari kujenga viwanda hapa nchini.

Maoni yangu: Wale wote walinaojiandaa kununua magari yaliyotumika kwa bei nafuu wafanye haraka kabla sera mpya haijaanza kutumika.
---
Wakati Kiwanda cha Magari cha Mahindra cha India, kikikusudia kuwekeza zaidi Sh10 bilioni nchini, Serikali inakusudia kufanya mapitio ya sheria ya uagizaji magari nje kwa lengo la kubana zaidi uingizaji wa magari yenye muda mrefu ili kulinda wawekezaji wa ndani.

Ujio wa kampuni hiyo umekuja zikiwa zimepita siku 25 baada ya Rais Samia kufanya ziara nchini India Oktoba, mwaka huu na kuwashawishi wawekezaji waje kuwekeza nchini.

Mahindra wanakuja nchini kufanya uwekezaji wa uunganishaji wa magari madogo kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania ya Gf Automobile inayofanyia shughuli hizo Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi ya ushirikiano huo, iliyofanyika jijini Da es Salaam leo, Jumanne Desemba 5, 2023, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema katika ziara ya Rais Samia nchini India, kampuni ya Mahindra iliahidi kuwa ya kwanza kuleta shughuli zao nchini.

Amesema kampuni hiyo imekuja kwa ajili ya hatua za awali na kwamba ndani ya miezi sita itaanza uzalishaji wa magari hayo nchini.

“Uwekezaji huu maana yake ni kazi kwa vijana wetu, kodi kwa Serikali na kuongeza uchumi kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla,” amesema Profesa Kitila alipokuwa akifafanua nini maana ya uwekezaji huo katika uchumi wa nchi.

Amesema uwekezaji huo unaenda sambamba na malengo ya Serikali katika kuvutia wawekezaji katika sekta ya magari magari nchini, hasa yanayotumia umeme, kwa kuzingatia Tanzania ina madini ya Lithium yenye uwezo wa kutengeneza betri za umeme.

“Ili kukamilisha hili, Serikali itaangalia upya sera yake ya uagizaji magari kutoka nje, kwa sasa unaruhusiwa kuingiza gari lolote hata kama limeshatumika miaka 100 unaruhusiwa kuingiza,” amesema na kuongeza;

“Lakini ili kulinda viwanda vya kuzalisha magari hapa nchini, huko mbele lazima tuangalie sheria zetu upya ili kuzuia baadhi ya magari ambayo yamechakaa na hivyo kulinda soko la magari la hapa Tanzania na yale yatakayokwenda kwenda nchi nyingine.”

Hata hivyo, licha ya kuruhusu magari yenye umri wowote kuingia nchini, kiwango cha tozo ya uchakavu kinatofautiana kutokana na mwaka ambao gari ilitengenezwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Januari 2021 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), utozaji ushuru kwa magari yaliyotumika, hutokana na umri wa gari kwa kufuata mwaka wa kalenda.

Kwa upande wa magari madogo yenye umri wa miaka minane hadi tisa tangu kutengezwa, pamoja na kodi nyingine, hutozwa ushuru wa bidhaa kwa asilimia 15 huku yale yenye umri zaidi ya huo, hutozwa asilimia 30.

Ushuru mkubwa zaidi umewekwa kwa magari yaliyotengenezwa muda mrefu kama njia ya kuvunja moyo uagizaji wa magari yaliyotengenezwa muda mrefu.

Naye Mkurugenzi wa GF Group, Imran Karmali amesema uunganishwaji wa magari hayo madogo nchini utasaidia kushusha gharama za uagizaji na kuwawezesha Watanzania kumudu gharama.

“Pia magari haya yatakuwa mapya. Hivyo kama malengo ya Serikali ni kusaidia viwanda vya magari viongezeke, ni vyema kuweka mazingira magumu kwa magari yaliyo na miaka mingi kuingia nchini,” amesema Karmali.

Amesema waliona fursa ya kushirikiana na Mahindra baada ya Rais Samia kutembelea India ndipo waliamua kutafuta kampuni kutoka nchini humo ili waweze kushirikiana nao.

Kampuni ya GF imekuwa moja ya kampuni zinazounganisha magari makubwa nchini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kubebea mizigo na kwa mwaka huu pekee hadi Oktoba wamezalisha zaidi ya magari 1000.

“Tunapokwenda kuanza uzalishaji wa magari madogo, tutaongeza pia idadi ya ajira zitakazozalishwa, kwa sasa watu 250 wameajiriwa huku 700 wakiwa ajira zisizokuwa rasmi,” amesema Karmali.

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri amesema ujio wa kampuni hiyo unaakisi ongezeko la uwekezaji lililoshuhudiwa kati ya Julai hadi Septemba mwaka huu ambapo mtaji wa zaidi ya Sh2.505 trilioni umewekezwa sekta mbalimbali.

Amesema uwekezaji huo ni mara mbili ya kile kilichokuwapo kipindi kama hicho mwaka 2022, Pia ni nusu ya uwekezaji ambao Tanzania iliupata kwa mwaka 2019 na 2020.

Aliwataka Watanzania kushiriki katika mageuzi ya kiuchumi kwa kutumia vivutio mbalimbali vilivyowekwa na Serikali kwa ajili yao ili waweze kuwekeza kwa urahisi zaidi na kupata ushirikiano.

“Watanzania wenye shule, kiwanja, jengo wanaotafuta wabia wa kuwekeza nao, sisi TIC tunapokwenda nje ya nchi kuhamasisha uwekezaji hatutamani kuona wawekezaji wanakuja kusimama kwa asilimia 100 tungependa kuona kilichotokea kwa Gf Automobile na Mahindra kinatokea kwa Watanzania wengi,” amesema Teri.
Tanzania Kuna uzalishaji upi wa ndani wa magari? Upuuzi
 
Serikali nayo inunue magari hayohayo ya mwekezaji ili kumlinda na ku-support uwekezaji.

Huyo muwekezaji mmoja hawezi kutosheleza hitaji la aina ya magari yanayohitajika nchini kiasi iwepo sheria ya namna hiyo.

Hata ingekuwa ni Toyota mwenyewe anakuja bado mahitaji ya trucks watu watahitaji kuagiza scania za 450,000Km odo ndiyo wanazimudu.

Tope la Hanang limejaa kwenye vichwa vya wenye dhamana.
 
Wangeenda kujifunza Rwanda wanachofanya. Wao Wana viwanda vya Magari huko kwao. So polepole wanaanza kuzuia uagizwaji wa mitumba.
 
Watengeneze tu lakini watayauza kwa nani. Kama kipato cha Mtanzania kinamruhusu kununua gari lililotumika. Nimeyaona magari ya mahindra hayana kiwango kama magari kama toyota, harrier, vanguard yaliyotumika.
 

India kwenyewe best selling cars Suzuki brand ndio inaongoza.

Katika top 10 selling cars 8 ni Suzuki models, brand za magari ya India ni mawili 2 tena zipo nafasi ya 6 na 9 (kama magari yao ni reliable hivyo siyangeanza kuaminiwa na wahindi wenyewe kwanza).

Soko lao la second hand cars lina value ya $24 billion na lina kadiriwa kufika $43 billion baada ya miaka 10.

Hawa ndio watu wakufanya Tanzania iweke ugumu wa kuagiza magari kweli.

Akili za viongozi wa Tanzania zina reflect wananchi, hata ukisikiliza wafanyabiashara wa Tanzania mtu akianza kuzalisha bati, vifaranga (au chochote) utasikia ohh serikali izuie imports inaua soko la ndani.

Concepts za free market ya choice, affordability ya mlaji, competition haipo kabisa.

Sasa hapo utamlaumu muhindi kupewa favourable condition au mapoyoyo yasiyo na uwezo tunayoyapa nafasi kushika sentive posts za nchi.
Umeeandika serious sana ila we know hayo ni matamko yakumfurahisha mwekezaji, Serikali yenyewe tu haiewezi kununua gari inaitwa Mahindra…hizi zitakua za ma Gabachori ambao kabla ya hapo walikua wanaimport from India.
 
Kwani lazima kuendesha magari? Baiskeli ni nzuri kwa mazoezi pia zipo pikipiki ndogo za umeme ni cheap na zipo nyingi siku hizi. Tunajaribu kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.
 
Hakika nimeshtushwa na Taarifa ya Serikali kuwa inataka kubana zaidi USHURU kwa Magari yaliyotumika (USED) ili Masikini Watanzania WASHINDWE KABISA kununua hayo Magari ETI wanunue MAGARI MAPYA ambayo kuna MWEKEZAJI Katoa Sh BIL. 1O ili kuanzisha Kiwanda cha MAGARI MAPYA.

Najiuliza ni Watanzania Wangapi wenye Uwezo wa kununua MAGARI MAPYA? Kama hata Mawaziri na Wabunge wetu nao kimbilio lao ni haya haya Magari Yaliyotumika (Used) Mwananchi gani atanunua GARI JIPYA?
USHAURI kwa Serikali.

Badala ya Kumlinda Huyo Mwekezaji Serikali iwaangalie Wananchi wake kwa kupunguza USHURU badala ya kuuongeza ili Masikini Wananchi Waweze kununua MAGARI YALIYOTUMIKA kwa wingi ila irekebishe Umri wa Gari toka Limetengenezwa ili kubana kuingiza Magari ya muda mrefu toka yametengenezwa.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Hili serikali letu hapana.
Juzi tu wamepitisha sheria serikali inunue magari ya aliyotumika kwa ajili ya taasisi za serikali,alafu wananchi wako unawawekea ngumu wanaunue mapya.
Hivi ni lini watanzania tutaoka tuseme hapana? Tuwakatae hawa watu. Wahuni,wezi hawana nia njema kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom