Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lete kwangu, Kuna dampo nalifahamu la kutupa scraper kama yako.Lol Wapige na marufuku ya magari ambayo yapo barabarani sasa ya below 2020 yanachafua mazingira…. Ila IST yangu ya 2006 ntatupa dampo la wapi?
Ma CCM wana fikra za Kichawi sana.Nchi hii imekosa viongozi sahihi
Kampuni hii inakuja Tanzania kuunganisha vipande "parts" vya magari yao. Hawa wanatafuta soko la magari yao , watanzania tutaadhilika kwa kulazimishwa kununua magari hayo ambayo kiwango chake cha ubora kinaweza kisiwe sawa hata na cha magari ambayo yametumika kutoka Japan.Ni wazo zuri. Muhimu tu hao wazalishaji wajikite kwenye uzalishaji wa magari yao kwa kuangalia consumer needs. Yaani bidhaa iendane na soko lililopo.
Siyo wazalishe magari na kuyauza kwa pesa kubwa, huku wanunuzi wengi wakiwa hawana uwezo wa kuifikia hiyo bei.
Na serikali iachane na zile kodi zake kandamizi. Haiwezekani gari liuzwe kwa mfano shilingi milioni 6 za Kitanzania, halafu serikali nayo inalitoza gari hilo hilo kodi ya shilingi milioni 6! Huu ni wizi, na pia ni dalili ya kuwakomoa wananchi.
Wacha nikapime chuma chakavu
Mbona umewalenga mwalimu ambao nchi hii hawafiki hata 600K. Mbona hata hali za watumishi wa kada zingine ni kizungumkuti tu. Hata hawa wafanya biashara ni wachache sana anaweza agiza gari mpya.Nafikiri hii sera ni maalumu kuwakomoa walimu,sasa mwalimu anaweza kununua gari jipya kweli
Tena zile zilizoletwa kwa ajili ya ccm na sidhani kama kuna yoyote bado iko barabaraniMagari yenyewe mahindra