Serikali kuweka sheria ya kuwabana wasiovaa maboya kwenye Vyombo vya Majini

Serikali kuweka sheria ya kuwabana wasiovaa maboya kwenye Vyombo vya Majini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Sheria kubana wasiovaa maboya yaja.

SERIKALI iko mbioni kutunga sheria itakayowaadhibu watu watakaopanda vyombo vya majini hususani mitumbwi bila kuvaa boya wakiwa baharini au ziwa lolote nchini.

Akizungumza wakati akitoa elimu kwa wananchi mkoani hapa katika Mwalo wa Ujaluoni, Lunazi, Kata ya Izumacheli juzi,

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Emmanuel Ndomba alisema, shirika limekuwa likitoa elimu kuhusu usalama wa watu wanapokuwa kwenye vyombo vya usafiri majini.

Alisema wameona kama ikiwapo sheria itakayomwadhibu asiyevaa boya, itapunguza vifo vitokanavyo na kutovaa vifaa vya uokoaji.

“Kuna umuhimu wa serikali kutunga Sheria, iwe ni lazima mtu yeyote anayeingia kwenye vyombo vya majini hasa mitumbwi, awe amevaa boya, kama itatokea mtu atakiuka ashtakiwe.

“Tutaishauri serikali, ikiwezekana kuwe na kanuni za adhabu ili mtu asipovaa boya, anapokuwa kwenye vyombo vya usafiri majini anapewa adhabu kali.
 
Kichwa kingekuwa "serikali kujipatia mapato kwa wasiovaa maboya" kingeakisi zaidi ile mitano tena 😂😂😂😂😂😂.
 
Back
Top Bottom