Rushwa inarudi kwa kasi Tanzania na inasikitisha sana. Serikali na viongozi wakuu kama wenyewe sio wala rushwa inabidi wafanye ufuatiliaji wa vitu vya wananchi. Nitatoa mifano hapa
1. Kama ni mfanyakazi wa serikali tujiulize ni kwanini card za NIDA zinachelewa? Ukiangalia vizuri hakuna tatizo lolote la card lakini watu wa NIDA wana zibania makusudi ili ukienda kuomba au kuulizia card yako utoe chochote. Tatizo kubwa viongozi wa juu wa NIDA na wenyewe ni wala rushwa wakubwa. Lakini cha ajabu viongozi wanaona hili na kunyamaza
2. Mabasi ya mwendo kasi kwa makusudi watu ambao wamewekwa kusimamia wanatafuta njia za kuharibu mfumo wa kutumia cad ili waweze kulipisha watu pesa bila kadi na kuweka pesa mifukoni kwao. Imefika sehemu serikali inataka kuweka kampuni ya nje kwasababu tu ya rushwa na mfumo wa rushwa kwenye haya mabasi!. Mpaka waziri mkuu anajua hili lakini bado ujinga unaendelea
3. Kwenye vibali vya umiliki wa viwanja yaani wamekuja na kisingizio eti hawana makaratasi maalumu ya vibali. Hivyo hupewi lakini ukitoa pesa tu unashangaa unapewa. Hivi ni vitu ambavyo vinafungiwa macho lakini ni muhimu sana wa wananchi na maendeleo.
Kuna barabara ya Arusha ya bypass watu hawaitumii kwasababu ya rushwa kubwa ya traffic na wameweka matuta kila mahali. Tatizo traffic wanapewa budget na wakubwa wao ya makusanyo ya rushwa kila siku. Serikali cha ajabu wanafungia macho vitu kama hivi. Mimi wasiwasi wangu mkubwa kwa serikali hii ni kurudi kasi kwa rushwa