Serikali kuzuia mazao ya chakula kuuzwa nje inakwepa majukumu yake na ni uonevu mkubwa kwa wakulima

Serikali kuzuia mazao ya chakula kuuzwa nje inakwepa majukumu yake na ni uonevu mkubwa kwa wakulima

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Moja ya wajibu mkubwa wa serikali ni kulinda na kudumisha usalama wa nchi. Usalama wa nchi huchangiwa kwa kiasi kikubwa na usalama wa chakula (upatikanaji wa chakula kwa bei inayohimilika).

Kinyume chake nchi inaweza kuingia ktk machafuko. Mfano, serikali ya Al Bashir wa Sudan iliondolewa madarakani kwasabb ya bei isiyohimilka ya mkate tu.


Serikali inapaswa kufanya nn ili kulinda usalama wa chakula?

Serikali makini inapaswa kujenga maghala makubwa ya kuhifadhia chakula kila kitongoji, na kila mtaa. Kisha kununua mazao hayo kwa bei ya sokoni toka kwa wakulima na kuyahifadhi.

Mataifa makubwa kwa mfano, mpk Sasa bado yana nafaka iliyonunuliwa na kuhifadhiwa tangu mwaka 2000. Ndiyo maana mnaona Ukraine Ina mwaka wa pili Sasa iko vitani lkn husikii kilio cha njaa. Hapa kwetu serikali Ina maghala ya kuhifadhi tani laki mbili za nafaka nchi nzima. Tani hizi we zinazotosheleza mahitaji ya nchi kwa mwezi mmoja tu. What a joke!!


Kwahiyo serikali imetumia njia ya mkato ili kujilinda kwa kuwaumiza wakulima. No! No! No!. Njia hii itaongeza idadi ya wadangaji, machawa na wanaobeti mjini. Kwasabb wakulima wanateseka halafu wanaocheza pull na kudanga mjini wanapata mazao kwa bei ya bure huku mkulima akipata hasara. Basi nao bora wakadange na kubeti.

Serikali jengeni maghala makubwa kila kitongoji na kila mtaa. Acheni kuonea wakulima.!¹
 
Njia ya kudumu zaidi ni kuwaondoa raia wake wengi katika umaskini wa kipato ili waweze kununua chakula wenyewe kwa bei za ushindani wa soko la kimataifa.
 
Wanazuia export ili kuua kilimo ili kuongeza tatizo la ajira nchini ili wengi wawe masikini wazidi kutawaliwa kwa kuhongwa kofia na t shirt
 
Inashangaza serikali kushindwa kutatua hili tatizo kwa miaka mingi sasa. Au tubinafsishe jambo hili nalo?
 
Sijui viongozi wetu wanawaza kutumia nini? Gharama za kilimo zimepanda sana, halafu unakuja kumzuia mkulima kuuza mahindi yake palipo na unafuu.
 
Sijui viongozi wetu wanawaza kutumia nini? Gharama za kilimo zimepanda sana, halafu unakuja kumzuia mkulima kuuza mahindi yake palipo na unafuu.
Hapa tunaua mitaji ya wakulima waliokopa benki ili kuwekeza kwenye kilimo na kuwafanya wakulima kuwa maskini daima
 
Back
Top Bottom