Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Serikali: Kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 66 wa Corona nchi nzima ndani ya mikoa 10 na mikoa 16 haina wagonjwa

Tatizo lako u aandika unavyotaka wewe ueleweke, lakini hakuna mtu amesema kuwa Coronavirus vimeisha Tanzania. Tuliyo yasikia wengi ni kwamba Covid-19 ipo na tuchukue tahadhari ambazo zimetolewa na wizara ya Afya.

Hiyo haitufanyi sisi tukakosa kufanya shughuli zetu za kujipatia kipato kama kawaida yetu.

Covid-19 bado ipo ila zile hofu ambazo WTO na wengineo walitutabiria kuwa tutaokota mizoga ya ndugu zetu barabarani a kwamba hospitali zetu zitaelemewa, hiyo haipo na haitakuwa kuwepo.

Tatizo hapa wenzetu wanatungumzia hali yetu wakati maisha yetu hawayajui.


Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana
 
Vya wahenga vizuri mkuu.Tafuta hicho kitabu ukisome ujue wahenga tulivyofaidi. Nikiwa mtoto wa level ya darasa la nne, kilinipa uelewa wa mambo mengi sana hadi walimu walinishangaa kwa maswali niliyokuwa nawauliza.
sawa no tatenga mda kwa ajili ya hilo
 
Kwa nini watu wanagomba na lawama tele kama zumbukuku kuhusu takwimu?

Kwa vipi takwimu ndio kiwe kigezo cha mtu kuzingatia ushauri wa kujikinga?

Kama wewe mwenyewe umeridhika kuwa COVID-19 imeisha acha kuzingatia kanuni za kujikinga dhidi ya maambukizi.

La

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO
 
Mbona JESUS alisema wapo wagonjwa wanne tu? Waziri Mkuu asitutafute maneno ngoja tusuburi ripoti ya Jesus mwenyewe hawa Mitume hatuwaamini Tena.
Kwahiyo JPM akiwa Jesus waziri mkuu atakua nani? Peter au ?
 
Serikali inasubiri nini kuanza kupima wananchi kwenye maeneo yao wanamoishi Kama nchi nyingine wanavyofanya? Mwisho wa siku tutakuwa tunasema tunawagonjwa kadhaa kumbe uhalisia tatizo ni kubwa.

Ushauri wangu;
1. Serikali izidi kuchochea wananchi waweke mbele tahadhari zaidi.

2. Kuanzishwa mkakati maalum wa ufuatiliaji kama nchi za Kenya na Rwanda walivyofanya kwa kuchukua sample kwa raia ngazi ya chini kabisa angalau kwa kuanzia kwa watumishi wa afya ili kupata picha pana zaidi ya hali ilivyo kwa nchi nzima.

3. Wizara ya afya iweke mikakati maalum na mahusus ya kudhibiti na kufanya cross check ya mara kwa mara Hadi pale ugonjwa huu utakapo pungua kabisa Kama Sio kumalizika katika nchi yetu na nchi za jirani. Ni ngumu sana kurelax endapo jirani yako wa karibu kabisa Kama Kenya anatapatapa kwa tatizo hilo hilo ambalo Tanzania tunalo na muingiliano baina ya nchi hizi mbili bado upo.

TUCHUKUE HATUA.


Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
 
Wanachowaza wao ni uchaguzi tu,

Kuaminisha umma kuwa gonjwa hatari limeisha kwa nguvu ya maombi kumbe porojo tu.
 
Back
Top Bottom