Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Waziri mkuu amesema magari yaliotengenezwa chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini, naona tunakoelekea kumiliki gari itakuwa ujipange haswa.

Na biashara ya magari yaliondani ya nchi inaenda kukua kwa Kasi.

Sidhani kama WM ana uelewa na uingizwaji wa magari. Naamini kakosea kuongea tu.

Kuna taratibu za uingizaji wa magari. Ukiingiza gari lenye umri mkubwa calculator ya TRA inakusubiri.
 
Pitia sheria zake utaelewa... hakuna gari lisilo la maana, sheria ilitungwa kwa nia njema labda kama utekelezaji una suasua mpaka mh. ameamua kuweka sawa
 
Magari mengi nchini ni kuanzia 2003 Hadi 2009 kuanzia 2010 ni machache sana kwanza hiyo Sheria Bunge ilishapitisha au ndio kila kiongozi anajiongelea tu
 
Sheria huwa haitaji mwaka husika (kama 2010 etc) bali hutaja umri (kama miaka 10 etc).
Sasa sijui waziri mkuu alilenga umri upi wa mwisho wa gari wa kuruhusu gari kuingizwa nchini.
 
Waandishi wetu wa habari hawajiongezi kutuelimisha sisi wasomaje. Sababu ya Serikali kupiga marufuku magari yaliyotengenezwa miaka 12 iliyopita ni nini?

1) Je Tanzania inageuka jalala ya kutupia magari chakavu,

2) je haya magari yanatumia teknologia ya zamani ambampo yakitembea barabarani yanatoa kemikali zinazochafua hewa na kuhatarisha maisha ya watu na mazingira,

3) haya magari yakingia nchini hayadumu hata miezi sita na inakuwa hasara kwa mnunuzi na nchi kwa kupoteza fedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza mahitaji mengine - kama madawa na chakula.
 

Yep, inabidi wafafanue, waulizwe wametumia vigezo gani? Kwa kiwango gani hii marufuku itaathiri sekta ya usafiri, usafirishaji na maisha ya Mtanzania kwa ujumla.

Mipango gani mbadala wameiweka kupunguza hizo athari?
 
Kama umeelewa hapo kwenye neno "uchumi wetu" basi wala usingeleta hoja ya kutokuijua serikali yetu.

Hapo nimeweka wazi kabisa uchumi huo hatujaufikia.
Kuwa na viwanda vya hayo magari hakukufanyi uweze ku-afford hayo magari.

Mnaweza msiwe na kiwanda hata kimoja ila mkawa na uchumi imara ambao wananchi wana uwezo wa kununua magari mapya.
 
Alicho kisema MH waziri mkuu ni kizuri, kwa sasa tunaona kama tunaonewa sababu tunahisi bei zipo juu itafika wakati tutaanza kuwaza brand nyingine kama Mazda, Nissan, Volvo, BMW, VOXHAUL n.k ambazo bei yake haijachangamka sana TOFAUTI na TOYOTA, hicho ndio kilichofanyika Kenya, Rwanda na Uganda ...Tulikuwa nyuma kwa muda mrefu sana
 
hapo mbona mbali wangefanya mwsho 2015
 
Huyo waziri mkuu wenu ni mmoja ya watu wanaoongoza kwa kutoa kauli ambazo ni lifeless, mwaka jana aliwaambia Mzee Magufuli yupo ikulu anakagua mafaili wakati mzee wa Watu yupo mbinguni tayari.

Kwa kifupi Katelephone ni msema hovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…