Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Serikali: Magari chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini

Mda umefika wa kujipanga kuipenda ist new model

Ila wangefanya 2000-2005 inge make sense

Nahisi toyota atapata upinzani mkubwa sana kutoka kampuni nyingine
 
Magari asilimia 80+ ni ya 2009 kushuka chini ha ha agiza crown ya 2011 [emoji1787][emoji1787]
kuna nissan xtrail model ya 2008 ile gari ni mkasi sana alafu bei mil15+ yani ile gari ndio imeanza kuingia alafu nayo ipigwe block kweli!!!
 
Mkuu Mheshimiwa PM MAJALIWA. NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA. NAKUPA EQUATION SIMPO SANA. UKITAKA MAGARI MIAKA 10 KUENDELEA NDO YAINGIE. PUNGUZA USHURU. HAIWEZEKANI MIMI KUNUNUA GARI LA MILLION 30 NATOA 30 NYINGINE YANI USHURU NI 100% HII SERA INAMSAIDIA NANI SASA? HAUWEZI PATA MAGARI 2012 KWENDA JUU KWA NAMNA HII. VIWANDA VYA MAGARI HAMNA, ASSEMBLY POINT HAMNAAA...SASA IWEJE.KODI NI 100% UNATAKA MAGARI 2012 KUENDELEA PUNGUZA USHURU
 
Kauli ya waziri mkuu sidhani kama inaweza kuwa sheria !! , Sheria inasema kuwa gari chini ya miaka kumi kutengenezwa inatakiww kulipa kodi ya uchakavu , dumping fees, sheria haikatazi watu kuagiza magari chakavu bali gari chakavu litalipiwa uchakavu wake .
Tamko la waziri mkuu kusema magari chini ya mwaka 2010 , linashangaza sana , na linakinzana na sheria ya bunge , Gari ya mwaka 2010 tayari ina miaka 12 , gari hii ni nzee tayari, lakini pia , ipi itakuwa ni base ya tamko hili? Kwamba na mwakani napo watatumia 2010 kama base ? Si linakuwa gari la miaka 13 ?
 
Nilitaka niagize RAV4 old model ya 1999 Kwa KAZI ngumu za nyumbani. Nimegundua hizi gari zina Engine ya 3s ni ngumu na engine kama roho ya paka. Yaani imekula kwangu
 
Fusso ya mwaka 1980 inasimamia Million 80+, je ya mwaka 2011 itakuwa ngapi?!
Hahahaha. Yaani mafisadi wamerudi wanajua wote Tuna pesa. Yaani Bora tumerudishwa tu loo inkamu kantri. Hivyo na magari wasilete hizo Sheria ni za Mido inkamu kantri.
 
Tumechelewa sana kuzuia nchi yetu kuwa jaa la mali chakavu.

Hapo Kenya tu uamuzi kama huu waliufanya kitambo sana na maisha yanasonga.

Kama kipato chako hakijafikia ngazi ya kununua gari, chukua chombo cha usafiri unachokimudu!
Mkuu
Ungeyajua maisha ya mkenya wa kawaida usingesema haya.
System ya kibepari inaondoa ndoto zooote za maskini, kenya wanaagiza magari chini ya miaka 8, , unaweza kupata picha ni tabaka lipi hapo linaongelewa , pro box ya mwaka 2015 kwa bei ya japan hadi ifike kenya ni watani wa dola 12000, unaongelea 30 plus milions tshs , wanagapi watamudu hii hapa kwetu?
 
Hayo ni maneno tu yatapita
Kuna sheria kabisa ya haya mambo na sijui kwa nini waziri hajataka kuliweka kisheria , ila naamini na media nazo zimemnukuu vibaya maana kwa kauli ile , ni kama hajui sheria inasemaje na akitaka kufuta inatakiwa hatua zipi zifatwe.
Sheria zilizotungwa bungeni haziwezi kufutwa kwa matamko
 
Massoud Kipanya ameshaanza kutengeneza.

Kila kitu Mchina naona
Yeye kachomelea body tu
Hivi kuna clip kamili ambayo warsha inaonyesha tangu anaanza mpaka anamaliza?
Maana mtu anatengeneza kitu lazima ana rekodi pia [emoji848][emoji848]
 
Sidhani kama WM ana uelewa na uingizwaji wa magari. Naamini kakosea kuongea tu.

Kuna taratibu za uingizaji wa magari. Ukiingiza gari lenye umri mkubwa calculator ya TRA inakusubiri.

Exercise duty due to Age
Haina Madhara kwa kuwa inakuwa charged on CIF na CIF ya magari ya miaka ya nyuma ni ndogo ndiyo maana hakuna mzigo wa gharama kwa mnunuaji.
Unaweza kukuta hiyo Exercise duty due to Age ya IST 2004 unalipia US Dola 860 Sasa hapo bado kuna unafuu sana kwa mnunuaji.
Haya magari ya kuanzia 2010 bei yake hata ya kununulia japan imechangamka sana.
Kumbuka kwa mujibu wa kikokotoo cha TRA kinapiga Exercise duty due yo age kwa magari yaliyotengenezwa miaka SABA kuanzia tarehe husika ya kuangalia ushuru(mfano Leo) kurudi nyuma.
Kwa mfano ukiagiza mwaka huu 2022 ili kuepuka Exercise duty due to age inabidi uagize gari la mwaka 2015 kuja juu.

Angalia hapa [emoji116]
IMG_7291.jpg

IMG_7289.jpg

IMG_7287.jpg
 
Hii kauli tunaweza kuichukulia poa lakini Kuna magari ya maana sana Hatutayaona tena yakiingizwa Nchini..
Haya yafuatayoView attachment 2181908View attachment 2181909View attachment 2181911View attachment 2181913View attachment 2181914View attachment 2181915
Magari Yoote haya yametengenezwa 2009 kurudi nyuma....

Siyo rahisi kutekelezeka kwa hyo kauli...

Sijui kama wanamaanisha kweli walichokisema
Kama ni hapa watajikuta hata kodi wataikosa....sasa kama magari hayo tuu hayaingii yataingia magari gani?
 
Idadi ya magari yanayoingia bandarini yatapungua sana ....watarudi kulialia kodi zimepungua bandarin.


Lets wait and see
 
Mkuu Mheshimiwa PM MAJALIWA. NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA. NAKUPA EQUATION SIMPO SANA. UKITAKA MAGARI MIAKA 10 KUENDELEA NDO YAINGIE. PUNGUZA USHURU. HAIWEZEKANI MIMI KUNUNUA GARI LA MILLION 30 NATOA 30 NYINGINE YANI USHURU NI 100% HII SERA INAMSAIDIA NANI SASA? HAUWEZI PATA MAGARI 2012 KWENDA JUU KWA NAMNA HII. VIWANDA VYA MAGARI HAMNA, ASSEMBLY POINT HAMNAAA...SASA IWEJE.KODI NI 100% UNATAKA MAGARI 2012 KUENDELEA PUNGUZA USHURU
Nakuunga mkono,serikali ukinunua gari lako na yenyewe unainunulia gari kama ya kwako,yaani ni pasu kwa pasu,ujinga gani huu?
 
Back
Top Bottom