Serikali: Mechi ya Simba na Yanga imeonesha elimu zaidi bado inahitajika kuhusu CoronaVirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
SERIKALI imesema changamoto ya kupeana nafasi kwa mashabiki walioingia uwanjani katika mchezo wa Simba na Yanga inaashiria elimu zaidi inahitaji ili kuchukua tahadhari ya janga la maambukizi ya virusi vya corona viwanjani.

Katika mchezo huo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, Serikali iliruhusu mashabiki 30,000 kati ya 60,000 wanaojaza Uwanja wa Taifa kuushuhudia mchezo huo 'live', kwa lengo la mashabiki kuachiana nafasi ili kuchukua tahadhari ya corona.

Hata hivyo ilikuwa tofauti, kwani licha ya baadhi ya majukwaa kuwa tupu, lakini mashabiki waliendelea na utamaduni waliouzoea wa kukaa karibu karibu uwanjani na kutoachiana nafasi.

Singo amesema "Imekuwa changamoto sana, bahati mbaya mashabiki wetu wamezoea kukaa pamoja, lakini wanahitaji elimu zaidi kipindi hiki cha tahadhari,"

Amesema mchezo huo umewafundisha kuweka mkazo katika kuchukua tahadhari na kuongeza kuwa katika mechi ya fainali ya kombe hilo ambayo itachezwa mjini Sumbawanga kuna uwezekano idadi ya mashabiki watakaoingia uwanjani ikapunguzwa zaidi.

''Simba na Yanga tuliweka idadi ya nusu mashabiki, lakini haikusaidia, kwenye fainali hiyo (Simba vs Namungo) kuna uwezekano hata hiyo ya nusu mashabiki ikapunguzwa zaidi," amesema.

Amesema watafanya tathimini ya mechi ya Simba na Yanga, kabla ya kuja na mkakati wa nini watafanya.

Kuhusu sabuni za kunawia mikono kukosekana katika mchezo huo, Singo amesema idadi ya zilizokuwepo zilizidiwa na wingi wa mashabiki.

"Wakati milango ya uwanja inafunguliwa, sabuni zilikuwepo, itakuwa ziliisha baadae, japo hiyo pia ni changamoto ambayo tutaijadili wakati wa tathimini," amesema
 
Uwanja ufungiwe tu Kama walivyofanya Dodoma na Mbeya
 
daaah.. huyo anatafutwa kutumbuliwa tu.. hajui kwamba Magu anataka ieleweke "koona" haipo
 
TFF wametoa idadi ya watu waliongia uwanjan, full mauzauza, wanasema watu walioingia uwanjani ni 22,000 yani robo ya idadi ya uwanja...
 
Hata hivyo ilikuwa tofauti, kwani licha ya baadhi ya majukwaa kuwa tupu, lakini mashabiki waliendelea na utamaduni waliouzoea wa kukaa karibu karibu uwanjani na kutoachiana nafasi.
Kwani kuna mtu ambar alitaraji tofauti na hivyo? Hakuna cha kustaajabisha kwa mashabiki kufanya hivyo kiatariatari zaid
Kuna big mech ingine hapo nyuma kidogo mambo yalikuwa kama hivyo tu so hakuna jipya.

Na sio hapo uwanjani tu bali hata ktk mabanda ya kuonyesha mipira takriban nchi nzima vijijini na mijini mikusanyiko style ndo hizo hizo!! Mi sijui kifuatacho. .... tunaomba viongozi wetu waingilie kati
 
Wapuuzi hao, mbona wao walibanana huko kwenye vikao vyao na mziki juu
 
Back
Top Bottom