Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

Serikali: Mgonjwa wa Corona afariki dunia Mloganzila Hospital

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa afya Ummy Mwalimu ametangaza kifo cha mgonjwa wa Corona kilichotokea leo asubuhi katika kituo cha Mlonganzila.

Anakuwa mgonjwa wa kwanza nchini kutangazwa kufa kwa ugonjwa huu.

"Nasikitika kutangaza Kifo cha Kwanza cha Mgonjwa wa COVID-19 hapa nchini Kilichotokea alfajiri ya Leo katika Kituo cha Matibabu ya wagonjwa wa COVID-19 kilichopo Mloganzila DSM. Marehemu ni Mtanzania Mwanaume Miaka 49 Alikuwa akisumbuliwa na Maradhi Mengine"

Waziri Ummy Mwalimu

IMG-20200331-WA0022.jpg
 
Kutoka kwa Waziri wa Afya Tanzania bara Ummy Mwalimu

Kifo cha kwanza kimetokea leo alfajiri hospitali ya Mloganzila na marehemu alikuwa mwanaume mwenye miaka 49 pia alikuwa na magonjwa mengine yaliokuwa yanamsumbua ambayo hayajawekwa wazi tunahimizwa kufata magizo na maelekezo ya kiafya yalioagizwa kwanzia hapo mwanzo #staysafe #vivatanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume wa miaka 49... Amepatwa na umauti Mloganzila leo asubuhi na pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine.

Kutoka kwa familia ya marehemu:

TANZIA

Familia ya Marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kwa huzuni kubwa inasikitika kuarifu msiba wa mdogo wetu mpendwa IDDI HASHIM MBITA uliotokea usiku wa kuamkia leo hospitalini Mloganzila.

Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake, CORONA, serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana. Wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi. Hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi. Kila mtu aomboleze kwake.

Dua nyingi tumuombee Iddi Allah amuweke pema peponi. Amina.
 
Watu mnaoendeleza maombi kwa Mungu bila kuweka jitihadi za kujinga dhidi ya huu ugonjwa mna feli wapi?

Nyie endeleni kujikusanya kwenye makanisa, misikiti, masoko, ofisini, bungeni na mikutano halafu mtapata mrejesho wake.
 
Back
Top Bottom