TANZIA
Familia ya Marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kwa huzuni kubwa inasikitika kuarifu msiba wa mdogo wetu mpendwa IDDI HASHIM MBITA uliotokea usiku wa kuamkia leo hospitalini Mloganzila.
Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake, CORONA, serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana. Wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi. Hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi. Kila mtu aomboleze kwake.
Dua nyingi tumuombee Iddi Allah amuweke pema peponi. Amina.