Serikali mhemko: Vyuo vyote vikuu Dar vimefungwa kupisha mkutano ya viongozi

Serikali mhemko: Vyuo vyote vikuu Dar vimefungwa kupisha mkutano ya viongozi

Leo tare 27.1.2025 serikali imefunga vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam kupisha suala la "Mkutano wa wakuu wa nchi" 🤧 pamoja na shughuli zingine za kiuchumi zimesimamishwa.

Fikiria kwa wanachuo wanaosoma DIT,NIT,IFM,TUMAINI, UDSM, ARDHI hadi ST. JOSEPH UNIVERSITY IN TANZANIA cha mbezi nacho kimefungiwa kufanya kazi kwa siku 2 hivi serikal imeona nini hadi kuzuia visiendeleze masuala ya kitaaluma?

Fikiria tu kwa siku hizi 2 ni kiasi gani raia wataathirika na suala la mkutano, barabara 9 kuu zimefungwa na zote hizo hutumika pakubwa kuingiza na kutoa raia mjini.

Huwa ninawaza sana na ni kweli kuwa TANZANIA TUNA SERIKALI DHAIFU NA VIONGOZI VIPOFU KUWAHI KUTOKE
Acheni tupumzke....kusoma nako kuna chosha....siku 2 tu kelele kibaooo je ingekuwa wiki 1.....kipindi cha Corona mbona tulipumzka mwez m1 kiliharibika nini?
 
Subiri baada ya huu mkutano Lucas atakavyokuwa anampamba mama yake na kububujikwa na machozi yasiyo kuwa na ukomo

Sema huu nao uchizi,unafunga taasisi za umma kisa mkutano?.Kama ni jambo la usalama au wepesi wa viongozi kutembea na magari yao(foleni)mbona hizo barabara zingefungwa tu pale misafara yao ikianza na wakimaliza wanaruhusu raia waendelee na mambo yao(Hovyo kabisa)
Ndio li nchi lako mkuu 🤣
 
Tisa kumi wamesitisha hadi usahili wa walimu wa kiswahili sababu ya huu mkutano ,, kweli hii nchi ni kichwa cha mwenda wazimu
Kwani hakujawai kufanya mkutano wa kimataifa Tanzania!! Mbona mara zote watu wanaendelea na shughuli za kila siku na mikutano inaendelea.
Duh aiseee
Huu ni ushamba na ukurupukaji kwa nchi yetu kwa kweli inashangaza!
Kwa ufupi (hasa kwa wale ambao hawajapita Barabara ya Nyerere hivi karibuni) ni kwamba ujenzi wa barabara hiyo ya mwendokasi haujakamilika kwa 100% na kuna maeneo yamefungwa kwa vizuizi, kuna maeneo mnashea lane mnaoenda na wanaokuja nk. Kwa hiyo hatua ya kwanza ilikuwa kuifunga barabara hiyo na nyingine, baada ya hapo kila mamlaka ikaangalia busara zake katika sekta yake, kwamba wanafunzi wanaotumia route ile wasimame halafu wengine waendelee, walimu na staff wengine wanaotumia route ile wasimame halafu wanafunzi wafike nk. Kabla ya hiyo ya Elimu ilitangulia ya Katibu Mkuu Kiongozi, so unaweza ukaona kuwa walikuwa sahihi
 
Back
Top Bottom