Serikali: Miji ya Arusha, Dar, Zanzibar na Dodoma kuipaisha Tanzania kuwa Kitovu Cha Utalii wa Mikutano Duniani.Ukumbi wa 2 kwa Ukubwa Afrika kujengwa

Serikali: Miji ya Arusha, Dar, Zanzibar na Dodoma kuipaisha Tanzania kuwa Kitovu Cha Utalii wa Mikutano Duniani.Ukumbi wa 2 kwa Ukubwa Afrika kujengwa

Serikali Imesema Inapanga Kuifanya Tanzania Kitovu Cha Utalii wa Mikutano Duniani ambapo Miji ya Arusha,Dar, Zanzibar na Dodoma itajengwa kumbi za Kisasa Ili kutimiza Azam hiyo.

Aidha Inatarajia kujenga ukumbi mkubwa wa Mikutano ya Kimataifa ambao utakuwa wa pili Kwa Ukubwa hapa Africa jijini Arusha Kwa jina la Mount Kilimanjaro International Exhibition Centre kuanzia mwaka huu.

View: https://twitter.com/TZEmbassyCN/status/1698724924758831191?t=sIGcW5K9wGNa8GtcLOqehw&s=19

My Take
Wapi Mwanza na Mbeya mbona Zinatengwa Kwa Kila kitu? Hakuna Hoteli Wala Viwanja vya michezo. Why Kila kitu ni Dar,Arusha,Dom na Zanzibar tuu?

--
International conference Tourism is becoming more potent in boosting Tanzania's global appeal, with the government, through the Foreign Affairs Ministry, stating that strategies are in the pipeline to make Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, and Zanzibar leading conference destinations in Africa.

Addressing journalists at the State House in Dar es Salaam, the Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Ambassador Samwel Shelukindo, said that President Samia Suluhu Hassan has decided to make Tanzania Africa's top choice in hosting international conferences.

He says so far this year, Tanzania has hosted/will host two big global conferences: Africa Heads of State Human Capital Summit back in July and the Africa Food Systems Forum to be hosted on September 5.

Shelukindo said that these conferences come with a host of benefits to the country, including foreign exchange, boosting tourism, increasing money supply, and also providing good exposure for Tanzania.

As a result, he says the government plans on expanding the Arusha International Conference Centre (AICC) and also plans on building more international conference centres in Dar es Salaam and Zanzibar. Tanzania will also build the second-biggest conference centre in Africa.

Source: The Citizen

Kanda ya ziwa wametoa naibu waziri mkuu, mbeya wametoa rais wa mabunge, nafikiri inatosha kwasasa
 
Hapo umeongea upuuzi gani? Umesoma nilichoandika? Hiyo section inayojengwa inapita kwenye mlima upi wa kuchimbwa?

Mifano niliyotoa umeelewa? Umewahi Safiri Nje ya Tanzania wewe au unapayuka tuu.

Mijitu kama nyie ndio mnaharibu Miji yetu na hamna hata akili ya kujiongeza.
Sijakujibu ila nimetoa maoni yangu kuongezea yako, JF iko kazi!
 
🤣🤣🤣🤣🤣
Ngoja kwanza ni cheke....eti watajenga....Kila wakati ni tutafanya hivi tokea zamani wanasena watajenga uwanja wa kisasa Dodoma...lkn wapi... Kuna wakati walisema watajenga Recreational center pale Dodoma lakini mambo yalibakia kwenye papers
 
Hivi Mwanza waliikosea nini hii serikali ! Mbona inatengwa sana ?

Mwanza ilibebwa sana na Magufuli wakati anakomesha Arusha na kilimanjaro .
Arusha leo hakuna hata stand ila mji wa utalii.

Mwanza wamepewa miradi mingi maradufu zaidii ya Arusha shida ni miradi ya kipumbavu.
Wakati jiwe anajenga international Airport porini chato mlikaa kimya mkaona ni sawa.
Wapi panahitaji international Airport kati ya mwanza na chato??
 
Unapfanya miradi ya kimkakati lazima una target faida ya hii miradi baada ya wakati au muda flani sasa watu wanaona labda ni fasheni kudhan Mwanza pangejengewa ukumbi wa mkutano badaya ya Arusha.
Ndugu zangu mwanza ndio imepata hotel1 ya nyota 4 wakati Arusha inazo zaidi ya 10.
Arusha inahudumiwa na international Airport na Mwanza haina. Ule uwanja wa chato ulikuwa white elephant. Kwa kweli Mwanza ina safari ndevu kuwa mji wa kimataifa kwa sabab hakuna pool factor.
 
Serikali inaiogopa sana Mwanza wanajua wakibust miradi mingi mikubwa ya kimkakati hata hicho ki dar chao kitakuwa underdog Kwa Mwanza we fikiria mbali na kutopewa sapoti ya kutosha lakini bado haishuki ilipo je ikipewa itakuaje? Kuna wakati inafikia hata kuomba kila kanda ijitegemee kimapato Ili tuoneshane umwamba zaidi
Hapo ndio mnadhihirishwa wasukuma mlivo vichwa maji kama mwendazake
 
Nyie kipindi cha magufuli hamkupata mradi wa barabara bora njia nne, hamkupata mradi wa maji wa bilioni 520, je hamkujengewa barabara kila kona? Au mnatama mradi wa meli, au mnataka mjengewe daraja kuunganisha mlima meru na mlima kilimanjaro? Au sgr kufika Mwanza mnaona nongwa? Kanda ya ziwa ilipendelewa kwa kipi?

Endelea na ujinga na chuki zenu hii mizizi mnayopanda itakuja kuligharimu hili taifa.
Hospital ya rufaa chato

International Airport Chato

University of chato
Mbuga ya burigi (jkwe project)
Kigongo busisi
Meli ziwa Victoria
Stand ya mkoa
Etc
Mkuu mradi wa maji mmoja ni kweli sawa na haya yote??
Barabara zipi zimejengwa Arusha na jwe?
 
Arusha bado ni mji uliokaa vibaya barabara nyembamba sana kuliko miji yote…ukiangalia ile stand ni aibu Arusha kuwa jiji kabisa! Serikali inapaswa kujenga stand kwa nguvu sio kuwaacha watu wabishane pakujenga stand toka enzi za JPM
 
Ila Watu wa Serikali mkome kudanganya ,hizi sio zama za Nyerere.

Ukumbi huo Mpya wa Arusha wenye capacity ya watu 3,500 unaweza usiwepo hata top ten achilia mbali uongo wa kusema utakuwa wa pili Afrika.

Bukifaso wanajenga Ukumbi mkubwa wenye uwezo wa kuchukua watu 5,000 Kwa pamoja Mjini Ougadougou.
Hahaha yani watu 3500 wanaona ni watu wengi! Baada ya kufikiria watu elfu 50+ wao wanawaza 3500 wakidhani ni wengi eti…,
 
Njia pekee ya kuyaepuka haya na kupunguza manung'uniko ni serikali kuu kuacha kiasi kikubwa sehemu husika angalau 80% ya mapato na 20% iende serikali kuu haiwezekani mahitaji na vipaumbele vya kila mkoa viamliwe na wachache, jiulize hata suala la International Airport tu imeshakuwa ni wimbo ukiagiza chochote nje ya nchi andaa na nauli ya kukitoa dar kukileta ulipo, pili unategemea utalii ukue sehemu zingine za nchi kwa kutegemea viwanja hivyo pekee? Hapa lengo sio kuoneana wivu lengo ni tukue kwa pamoja kwani kuna ubaya gani kubolesha huko na huku kwetu napo pakaboreshwa yaani ni sawa sawa usomeshe watoto wawili watatu uwaache alafu uwakutanishe kwenye mtihani mmoja, hii sio fairy hata kidogo serikali ni influencer mkubwa kwenye mambo ya maendeleo na fursa endelevu why iwe kwa baadhi ya mikoa tu?
 
Mnaonaje kama Dar, dodoma, arusha na zanzibar mkiwa nchi moja , na sisi wamikoani tukijiundia serikali yetu? Kozi nyie mnaumuhimu kuliko mikoa yote heri muanzishe nchi yetu na sisi mikoa ya kajamba nani tuwe na serikali yetu.
Hiyo ndo miji ya Kimataifa. Huko kwingine ni miji ya Tanzania.
 
Arusha bado ni mji uliokaa vibaya barabara nyembamba sana kuliko miji yote…ukiangalia ile stand ni aibu Arusha kuwa jiji kabisa! Serikali inapaswa kujenga stand kwa nguvu sio kuwaacha watu wabishane pakujenga stand toka enzi za JPM
Ni kweli barabara kuu ile kwa mji kama Arusha ni fedheha pale Babylon au library ya mkoa hadi summit center hata kuvuka huwezi.
Stand ilikwamishwa na siasa za ubaguzi wa awamu ya mwendazake. Nadhani kwa sasa changes zimeanza kuonekana hata huo uwanja lazima utakuja na miundombinu mingine
 
Back
Top Bottom