Serikali mkililea hili kundi msije kulaumu huko mbeleni

Serikali mkililea hili kundi msije kulaumu huko mbeleni

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Kuna kundi linajitangaza eti wao ni WAVAMIA VIWANJA.

Kwenye mitandao ya kijamii kundi hili hu comment kwenye baadhi ya mada wakihamasisha wanachama wao waende kuvamia maeneo kadha wa kadha.

"...umoja wa wavamizi wa maeneo unawatangazia wanachama wote twende tukavamie mahali fulani kuna eneo zuri lisilo endelezwa kila mwanachama aambatane na sururu, panga, chepe, kiberti na mifuko ya foronya kwa ajili ya kuchomea nyasi tutakozo kusanya."

Huandika kundi hilo.
 
Aisee ni hatar, mwisho wa siku wanakuja kununua hivyo viwanja tena ilihali na maendeleo wengne washayafanya.
 
DSM - madale/goba, Chasimba - pale karibu na Kiwanda cha Cement / Bagamoyoo - Kiaraka / Mapinga / Tungutungu etc ---- ukitaka elewa matatizo ya uvamizi wa ardhi - tembelea mahakama ya adhi Kibaha

changamoto ni kwamba miji inakuwa kwa kasi, na kuna mwananchi mmoja ama familia inamiliki heka zaidi ya 50.
 
Kitendo cha kutengeneza makundi ya kuvamia maeneo siyo cha kiustaarabu, kwani mtu binafsi huwezi kwenda sehemu kwa utaratibu ukapata ardhi hadi ujiunge na makundi ya kuvamia. Mbona ardhi nchi hii bado ni kubwa sana......watu wa aina hiyo wanahatarisha amani, siyo wa kuwafumbia macho.
 
Hao ndio Panya rodi wa viwanja.
Ila tusisahau wapo pia mafisadi wanao dhulumu raia Kwa kutumia nafasi zao kuwabomolea nyumba na kuvuruga uendelezaki wa viwanja vya raia wanavyodai ni maeneo yao makubwa wanayomiliki kihalali,Ilhali SI kweli ila ujanja ujanja TU🤔
 
Back
Top Bottom