YAGHAMBA
JF-Expert Member
- Aug 8, 2012
- 545
- 147
Wakuu jana na leo gari la matangazo limekuwa likipita mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza na vitongoji vyake likitangaza tangazo la serikali ya CCM la kuwaamuru wamachinga wote, mama ntilie na wote wa kufanana nao kuondoka katikati ya jiji na sehemu zote 'zisizoruhusiwa' kabla ya siku ya jumatatu tarehe 15 Aprili 2013.
Tangazo hilo lenye vitisho vingi vyenye mwelekeo wa kuwadhuru wale wote watakaokaidi amri hiyo, limekuwa gumzo kubwa hapa jijini miongoni mwa wamachinga na wananchi wote kwa ujumla huku ikileta hofu kubwa ya kutokea maafa makubwa ikiwa litatekelezwa kwa namna ambavyo maneno ya tangazo hilo yanavyotamkwa na mtangazaji.
Mtangazaji amekuwa akisema kauli hizi " Kama unaipenda familia yako tii amri hii ya kuondoka ktk eneo unalofanyia biashara za umachinga kwani operation hii itakuwa kubwa na haina msalia mtume" na manenon mengine mengi yenye kutia hofu.