Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Wakuu,
Kipande hiki cha barabara ni maeneo ya Mbezi Beach Dar upande wa chini, ambako si mbali sana kutoka ilipo supermark ya Shopaz (kwa ambao si wenyeji wa maeneo haya), kipande hiko cha lami kinachoonekana hapo mwisho kwenye video ndio kinashuka na kupita ilipo supermarket ya Shopaz.
Sehemu hii DAWASA walikuwa na matengezo katika mfumo wa majitaka, (ambako nadhani ndio imesababisha maji Mbezi Beach kuwa na vumbi pamoja na harufu mbaya, niliweka uzi kuhusu hili, mpaka leo hii maji bado yana vumbi na harufi mbaya - Maji ya bomba yanazidi kuwa machafu kadri siku zinavyokwenda, DAWASA maji haya yana usalama kweli?) kuna bomba limekatika hapa ambako linafanya maji yavuje kidogo kidogo.
Kutokana na kuwa barabara haipitishi watu tu bali pia na magari ya uzito tofauti tofauti, panachimbika kadri siku zinavyozidi kwenda.
Kama mnavyoona mashimo yalivyo, kadri siku zinavyosonga yanazidi kuwa makubwa, mwisho wa siku barabara hii itakuwa haipitiki kabisa.
Lakini, nini kiliwashinda kuweka lami kwenye kipande hiki chote? Hizi kodi mnatukata kila pahala zinafanya nini kama miundombinu ni mibovu hivi?
Kama nilivyosema awali DAWASA walikuwa na matengezo kwenye mfumo wa maji taka maeneo haya mpaka kufika upande ule wa Dr. Hiza, barabara zilifumuliwa ili kukamisha ujenzi na maboresho yao.
Kwenye kipande hiki cha video ni eneo moja wapo (ambacho ndio kinatokea Shopaz), sehemu hii ni ya udongo mfinyazi ambako ikipata maji kidogo tu panakuwa natope la nguvu, yaani panaakuwa hapapitiki kabisa.
Sasa DAWASA walivyomaliza chimbachimba yao hata hawakujiongeza, wakarudishia udongo vile vile! Tunajua maji yakikutana na udongo hali inakuwaje, walishindwa kuweka lami basi wangemwaga zege au kuweka kokoto all the way through.
Mvua ikinyesha hapa ni tope kote, hii ni kero kubwa si tu kwa wenye magari lakini pia hata kwa watembea kwa miguu, vile vi udongo mlikuja mwaga juzi si lolote si chochote na majua hilo.
Acheni kufanya mambo kwa kulipua, mnatukamua wananchi kwa kodi kila sehemu, basi tuone kodi zetu zikifanya kazi, siyo kila sehemu tunapumulia mashine.
Hivi ndivyo panavyoonekana mvua ikinyesha, hiki ni kimvua kilichopita juzi hapa, sasa pata picha mvua inyeshe ka siku moja tu bila kukata hii sehemu itakuaje?
Sehemu ya Dkt. Hiza mpaka kufika Makonde, tena kuelekea Makonde nimeambiwa ndio balaa, nitaleta picha nikipita maeneo yale kama mtakuwa hamjaona huu uzi na kufanyia kazi. Serikali wajibikeni tafadhali, mnatuangusha sana wananchi.
Update
Dawasa wametengeza palipokuwa na shida, zaidi soma: Shukran DAWASA kurekebisha palipokuwa na shida hadi kutengeneza shimo, TARURA lini mtakuja kuweka lami/zege maeneo ya Mbezi Beach kwa Dr. Hiza?