Serikali mnusuruni Mandonga

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
798
Reaction score
1,178
๐Ÿ‘‰Pambano la Mandonga Zanzibar lifutwe ๐Ÿ™…

Hivi kweli Chama cha Ngumi Tanzania viongozi wao wanaelewa vyema sheria za mchezo huo?

Ndugu zangu Watanzania bara na visiwani, hivi kweli Mandonga anastahili kuangaliwa tu na kuachwa acheze mchezo huo,bila kuzingatia hali yake?

Kwanini Mtanzania huyu haonewi huruma? Mandonga anafanya mapambano bila ya kupumzika, kwamba haichukui muda akimaliza pambano hili, mara unasikia wiki ijayo anaenda kupigana na Bondia mwingine.

Chama cha Ngumi wanamtambua Bondia huyo lakini na wanamfwatilia?

Ni jambo la kusikitisha sana, nimeambiwa Mandonga anatarajiwa kufanya pambano visiwani Zanzibar tena ๐Ÿ˜ฅ

Mimi nashauri kama Mtanzania kuwa serikali imzuie Mandonga kwanza asicheze, sio kwakuwa hafai kucheza mchezo huo, lakini inawezekana Mandonga anahitaji elimu zaidi juu ya mchezo huo.

Tukumbuke Mandonga ana familia ambayo inamuhitaji na mchezo huo ni wa hatari. Vipi Mandonga aje afie Ulingoni?

Ahsante sana.
 
Nasikia kabla ya hilo la Zanzibar, ameandaliwa pambano lingine, akishapigwa ataelekea Zanzibar kwa ajili ya kwenda kupigwa.
 
Ndonga atakuja kuuawa yule, muda ambao angeutumia kujiandaa na pambano yeye anautumia kutoa tambo. Pole yeke...
 
Mandonga sio bondia hata yeye analijua Hilo ni.comedian .
Hakuna Bondia anayepigana kila wiki..
Na jinsi alivyokuwa kiazi anaachia tu uso ili ngumi ziingie vizuri.
Baada ya muda ataanza kupata matatizo ya ubongo maana ngumi zinaingia Sana usoni na huwa anaanguka Kama kiroba

Mapambano mengine hata hayatambuliwi na chama Cha ngumi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ