Serikali mpya ya Syria inajipanga kurejesha mahusiano na nchi za magharibi huku ikiipa Iran mkono wa kwaheri

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
14,885
Reaction score
18,083
Ufaransa yarejesha bendera katika ubalozi wa Damascus huku mamlaka mpya ya Syria ikijenga mawasiliano na nchi za Magharibi.

Ufaransa ilipandisha bendera yake katika ubalozi wake wa Damascus siku ya Jumanne kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12 na maafisa wa Umoja wa Ulaya walijitayarisha kuwasiliana na uongozi mpya wa Syria, ikiwa ni ishara ya kuongezeka kwa mawasiliano baada ya Bashar al-Assad kuondolewa kama rais.

Mataifa ya Magharibi hatua kwa hatua yanafungua njia kwa mamlaka mpya huko Damascus inayoongozwa na Hayat Tahrir al-Sham na kiongozi wake Ahmed al-Sharaa, ingawa bado wanaendelea kulitaja kundi hilo kama la kigaidi.
=================
France raised its flag at its Damascus embassy on Tuesday for the first time in 12 years and European Union officials prepared to engage with the new Syrian leadership, a sign of the growing contacts after Bashar al-Assad was ousted as president.
Western states are gradually opening channels to the new authorities in Damascus led by Hayat Tahrir al-Sham and its leader Ahmed al-Sharaa, though they continue to designate the group as terrorists.

https://www.reuters.com/world/middl...ntacts-with-syrias-new-leadership-2024-12-17/
 
Dah nafuu waachane na ugaidi maana Iran aliwafundisha mchezo mchafu
 
Kwani ni lini Syria iliwahi kukatisha mahusiano na nchi za Magharibi?

Nchi za Magharibi zenyewe ndo zilikata mahusiano na Syria baada ya vita kuanza.
Huyo Ufaransa mwenyewe yuko hoi baada ya kuporwa vibaraka wake wote Afrika Magharibi na Urusi.
 
Ebu acha kutuchekesha mleta taarifa.ivi kwa akili yako muungano wa Islamic state, Hayat Tahrir al-Sham na alqaida unaweza kweli kukaa meza moja na mataifa ya ulaya na wakaelewana hata tu mwaka mmoja.
 
Israel imetakiwa iharakishe na kuhakikisha imeripua silaha zote na bituo vyote vya Iran ili Syria ianze kujenga nchi na mabalozi waanze kurejea.
 
Israel inatekeleza hilo kwa umahiri mkubwa sana! Soon vyote vitageuka majivu.
Amelichekecha lile ghala la kuwekea silaha la Russia nchi yote imetikisika watu wakijua ni tetemeko la ardhi.
Ila ukiliangalia hili la Syria ndiyo utajua kuna watu wanafanya vitu kwa akili za kuona mbele sana.
Israel amesababisha Iran aliyekuwa akijidanganya na kudanganywa kuwa ni superpwer, sasa wanajiona kama Panya road tu. Kapiiigwa kipigo cha kimya na kuachwa amesimama, mashabiki wanazidi kumjaza wakimshangilia, wakashangaa kadili siku zinavyoenda anatepeta, anakaa chini na kudondoka chali.
Iran huyu aliyejifanya kuingilia Hezbollah kushambuliwa mpaka leo hajatia neno lolote tangu kutandikwa, kusambaratishwa hezbollah na silaha na vituo vyake kuteketezwa Syria.
 
Hii si habari mpya. Syria ndo itakuwa njia ya kupitisha mabomba ya NATURAL GAS kutoka QATAR kwenda jumuiya ya Ulaya. Gesi ya mrusi imeshakosa soko sasa. Poor RUSSIANS wa TANDALE KWA TUMBO
 
Kwani ni lini Syria iliwahi kukatisha mahusiano na nchi za Magharibi?

Nchi za Magharibi zenyewe ndo zilikata mahusiano na Syria baada ya vita kuanza.
Huyo Ufaransa mwenyewe yuko hoi baada ya kuporwa vibaraka wake wote Afrika Magharibi na Urusi.
Nchi gani inaizidi Ufaransa hiyo unayoisema ipo hoi? Yaani Ufaransa ilikuwa inaitegemea hizo nchi masikini za Afrika magharibi? Umeniuzunisha sana kwa hoja tako hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…