Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Nimehudhuria kliniki kwa ajili ya mwanangu kwa miaka miwili sasa sijawahi kukutana na elimu ya malezi ya aina yoyote ile kwenye hii kliniki, kinachofanyika ni kupima uzito mtoto au kuchomwa sindano ya chanjo kwa mtoto tena bila maelezo ya kwa nini mtoto apate chanjo wala umuhimu wake.
Sote tunajua jinsi ilivyo changamoto kwenye kulea Watoto, mama anahitajika kuwa na taarifa sahihi na kwa wakati juu ya nini ampatie mtoto wake na kwa wakati gani. Imezoeleka ili mama apate elimu ya malezi lazima ahudhurie kliniki apate elimu kutoka kwa wauguzi, ambao mara nyingi wamekuwa wanashindwa kutoa elimu kulingana na kuzidiwa na majukumu yao hivyo kuishia kutoa chanjo na kuwapima uzito Watoto na kisha kuwaruhusu waondoke.
Wazazi wanapata tabu kuuliza baadhi ya changamoto wanazokutana nazo wanauliza kwa wazazi wenzao au wazazi wao na kupewa majibu ya mazoea ivyo watoto kuendelea kulelewa kienyeji au kwa taarifa zilizopitwa na wakati.
Kwa mfano mpaka leo bado wazazi wanaamini mtoto akiwa na mwili mnene akisifiwa na watu wengi wapo wenye mdomo mbaya watamfanya akonde ivyo wanamfunga kitandaa cheusi aidha mkononi au kiunoni ili asikonde kumbe hapo ni swala la mtoto kupata lishe bora na kuthibiti asipate magonjwa yanashambulia watoto chini ya miaka 5 ndio suluhisho na haina uhusiano na kusemwa na watu. Vitu kama hivi ilitakiwa kupewa elimu kliniki ila hatupewi wazazi.
Elimu ya afya ya malezi ya Watoto kwa mwanamke ni muhimu sana ili aweze kulea mtoto wake kwa kufuata kanuni, taratibu na mtoto aweze kukua kwa afya ya mwili na akili hatimaye aje kulifaa taifa.
Dijitali yaweza kuwa suluhisho
Kwa kuwa imekuwa changamoto wazazi kupata elimu kwa wakunga basi wazazi watumie mitandao kusoma taarifa zinazohusu malezi ya Watoto kupitia mitandao kwa kuwa kadri siku zinavyokwenda watu wengi wanazidi kuwa na simu janja hivyo elimu itawafikia kwa wakati na popote watakapokuwepo. Hivyo wakienda hospitali wauguzi watajazia tu iwapo msomaji hakuelewa au ana swali Zaidi akihitaji ufafanuzi.
Mitandao imesheheni taarifa nyingi na elimu nyingi kuhusu malezi ya Watoto, nini Watoto wale ili wapate afya bora nini watoto wasile kulingana na umri wa mtoto husika, elimu hii ilikuwa ili kuipata ni lazima mama akutane na wauguzi ambao wanashughulika na kuangalia afya za Watoto na wakati mwingine inakuwa ngumu mama kupata elimu kwa kuwa wauguzi wanakuwa wamesongwa na msongomano wa Watoto lakini mama akiwa na mtandao na akaelekezwa kuwa atapata taarifa hizo ni rahisi yeye kuzipata akiwa nyumbani tu.
Wizara ya afya inaweza kuanzisha tovuti kwa ajili ya (Baba, Mama na mtoto) na kuwa wanasasisha taarifa na elimu mpya humo kwa wakati. Elimu kama mtoto anatakiwa kunyonyeshwa kwa muda gani, mtoto akipata dalili za kuumwa apelekwe hospital asipewe dawa bila kupima nk Taarifa zote, elimu zinakuwa zinapatikana kwenye tovuti hiyo ambayo mzazi ataambiwa kuwa kuna tovuti ya baba mama na mtoto ambayo ina elimu kuhusu malezi ya mtoto.
Hii itasaidia Zaidi kwa Wanawake (mama) waliokosa elimu kliniki kuendelea kuipata huko nyumbani na kusaidia watoto kukua kwa afya.