Serikali, msibane sana uhuru wa kufuga. Si kila kitu lazima kiwe "nyara za serikali"

Serikali, msibane sana uhuru wa kufuga. Si kila kitu lazima kiwe "nyara za serikali"

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
2,175
Reaction score
4,181
Tuwacheni msamiati wa nyara za Taifa hapa Tanzania, mbona tunaposafiri roho zinatuuma, unaona watu wanafuga kanga, unaona watu wanafuga paa, swala, digidigi unaona watu wanafuga tausi, vitu ambavyo vinahitajika kutaka kuongezwa katika generation ya Mtanzania.

Watz hatutaki kufuga simba wala chui au tembo (Hawa nao hufugwa India Tembo hutumika mitaani katika shuguli mbalimbali).

Tanzania leo ukikamatwa na ndege aina ya Kanga imeshakuwa kosa kubwa sana la serikali kutaharuki, kuandikwa magazetini waziri na mabwana pori kukutana na vyombo vya habari nini?

Mtanzania amekamatwa anafuga kanga mmoja usikute kanga mwenye kiguru.

Hebu tuvukeni katika baadhi ya mambo ukikamatwa na bundi Mtihani. Tukiambiwa Watanzania ni watu wa ajabu saa ingine tukubali tu.
 
Home kwangu kuna vijamaa vinaitwa vi karunguyeye, mida ya saa moja moja vinakuwaga vingi mno vijamaa havina shida na mtu ila shida ipo naogopa kuzoeana navyo nisije pewa kesi nzito.
 
Wenzetu wanafuga fisi kwa ajili ya kurahisisha usafiri na pia katika kucheza ngoma zao za asili. Kimbembe ni pale wanapokutana na Maafisa wa Maliasili, hukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kukutwa na Nyara za Serikali. Tuiombe Serikali kuangalia kwa umakini hizi sheria ambazo huwakwaza wananchi katika shughuli zao za kiutamaduni.
 
Back
Top Bottom