Serikali msitake kiki kwa askari wawili wa barabarani walioonekana wakipokea rushwa. Mifumo ya rushwa mmeasisi wenyewe

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mimi nachukia rushwa sana, na suala la rushwa kwa trafiki polisi nimelikemea sana humu JF na kwenye mitandao mingine.

Ila nachukia zaidi mtindo wa viongozi kujifanya watendaji bora na wasafi pindi inapoibuka video.

Pia soma Trafiki wawili wakamatwa baada ya kunaswa kwenye video wakipokea Rushwa hadharani

Hii imekuwa common sasa. Uozo kila sehemu, mahospitalini, kwenye sekta ya elimu, maji, umeme n.k
Hakuna kiongozi anayejali.

Hakuna uwajibikaji ila ikitokea kavideo tu viongozi lazima waitishe press na kuwafedhehesha wahusika.

Matrafiki kula rushwa imekuwa rasmi sasa, serikali imeshindwa kuwadhibiti, kwanini hawa wawili waonewe?
Serikali ingekuwa na nia ya dhati rushwa barabarani zingeisha miaka 10 iliyopita.

Sasa kila daladala asubuhi lazima itenge sh. 10-15 elfu ya rushwa barabarani.

Hatuyaki unafiki, acheni mihemko kwa kuhangahika na mambo ya kwenye video za mtandaoni.
Je, kama vimetengenezwa?

Kama kuna wahusika humu kateni rufaa, uchukuaji wa picha una Sheria na kanuni zake. Kama nchi hatuwezi kuenenda kwa video za mtandaoni. Ushetani kabisa.
 
Kweli kabisa.

Ni vigumu Sana kumpata Askari Polisi ambaye hajawahi kujihusisha na Rushwa katika nchi hii, labda yule ambaye ameajiriwa Jana au leo ndani ya Jeshi hilo.

Miaka fulani hivi ya huko nyuma ilikuwa Askari Polisi ili upandishwe Cheo ilikuwa ni kumkumbuka 'Bwana Mkubwa' kwa kumjengea nyumba na kisha unamualika aje au atembelee kwenye eneo lako la kazi na unamkabidhi funguo zake za nyumba. Siku chache baadaye Askari Mtoa rushwa ya nyumba anakuwa amepandishwa Cheo, wengi Sana walipanda vyeo kwa njia hiyo, na huyo 'Bwana Mkubwa' ana majumba mengi sana yametapakaa kwenye mikoa karibia yote hapa nchini, Wananchi wengi Sana wanafahamu suala hili na Askari wengi Sana (baadhi ya Askari wengine wakiwamo na baadhi ya Marafiki zangu wa karibu na/au Classmates wangu hadi leo hii wanamshukuru Sana huyo 'Bwana Mkubwa,' na wanaendelea kumkumbuka Sana tu).
 
Duuuuh
Huyo bwana mkubwa yuko hai?
 
Baadhi ya "vijiwe" vya kula rushwa za barabarani:-
1.Mbezi njiapanda ya Makabe
2. Goba center jirani na wauzaji wa samaki
3. Wazo Bwawani
4.Vingunguti mataa
5.Mlimani city opposite na kanisa la kakobe
6.Mikocheni mitaa ya clouds
7........

endelea
 
Kila mahali ambapo kuna trafiki polisi hicho ni kijiwe cha rushwa
 
Rushwa imetapakaa kila Mahali katika nchi hii ya Tanzania, hakuna kitu cha ajabu hapo. Ni Askari Polisi wachache Sana kupita kiasi ambao ni wasafi, Yaani hawajihusishi na Rushwa Wala vitendo vingine viovu vya uhalifu ama uvunjaji wa Haki za watu.

Kwa uzoefu wangu, kwenye kila penye Kituo cha Polisi jirani ya hicho Kituo lazima kuna Vijiwe vya kupokea rushwa au kuna Mawakala wa kupokea rushwa ili baadaye mzigo huo wa rushwa uweze kufikishwa kwa Askari Polisi anayehusika.
Mathalani, Mawakala ambao mara nyingi Sana hutumika kupokea rushwa za Maaskari Polisi na/au Mahakimu wa Mahakama huwa ni:-
1. Wapiga brashi Viatu ambao vilinge vyao huwa vipo jirani au pembezoni mwa Vituo vya Polisi.
2. Wauza Magazeti (ambao wapo katika vijiwe, fixed location).
3. Wahudumu wa Utoaji wa huduma Stationery au kupiga photocopies waliopo jirani na Vituo vya Polisi au Mahakama.
3. Askari wa Polisi Jamii au Askari Mgambo ambao wapo katika baadhi ya Vituo vya Polisi.
Mara nyingi sana Watu hawa (Polisi Jamii au Mgambo) hutumika kupokea rushwa za Maaskari Polisi na kuwapelejea wale Askari Polisi ambao wana Vyeo vya juu kidogo,
Kwa upande wa Mahakimu, wanaotumika kupokea rushwa zao mara nyingi ni wale Warumishi wa Mahakama wa ngazi za chini au wakati mwingine huwa pia kupitia kwa Mawakili.

Taarifa hii ni kutokana na Utafiti wa kificho Sana uliofanywa kuhusiana na masuala haya.
 
hawa maskari nao mananga sana.hatakama wakubwa wana kamisheni yao,ndio ukapokee rushwa kizembe hivyo. askari makini anajifunza mbinu za mashambulizi pamoja na wizi.sasa utafanyaje shambulizi bila kusoma mazingila..!
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hatari sana, tuanze kuwakamata wala rushwa wakubwawakubwa kwanza, tukifanya hivyo hizo ndogo zitakufa silent death
 
Baadhi ya "vijiwe" vya kula rushwa za barabarani:-
1.Mbezi njiapanda ya Makabe
2. Goba center jirani na wauzaji wa samaki
3. Wazo Bwawani
4.Vingunguti mataa
5.Mlimani city opposite na kanisa la kakobe
6.Mikocheni mitaa ya clouds
7........

endelea
Kisarawe, Masaki kwenye mwembe
 
Baadhi ya "vijiwe" vya kula rushwa za barabarani:-
1.Mbezi njiapanda ya Makabe
2. Goba center jirani na wauzaji wa samaki
3. Wazo Bwawani
4.Vingunguti mataa
5.Mlimani city opposite na kanisa la kakobe
6.Mikocheni mitaa ya clouds
7........

endelea
J4 yeye anapelekewa Ofisini kabisa mgawo wake...
 
Kama wala 'rushwa ndogo' mnata wasikamatwe basi hata vibaka wadogo kama pickpockets au wezi wa kuku nao wasikamatwe wawindwe tu wezi wa mikataba hewa ya mabilioni.
 
Baadhi ya "vijiwe" vya kula rushwa za barabarani:-
1.Mbezi njiapanda ya Makabe
2. Goba center jirani na wauzaji wa samaki
3. Wazo Bwawani
4.Vingunguti mataa
5.Mlimani city opposite na kanisa la kakobe
6.Mikocheni mitaa ya clouds
7........

endelea
Kwa kifupi ukiona trafiki Polisi ujue umeona Rushwa nyeupe.
 
Wanafukuza wote labda. Magazeti yamepata cha kuandika. Kuna hawa wengine
Your browser is not able to display this video.
 
hawa maskari nao mananga sana.hatakama wakubwa wana kamisheni yao,ndio ukapokee rushwa kizembe hivyo. askari makini anajifunza mbinu za mashambulizi pamoja na wizi.sasa utafanyaje shambulizi bila kusoma mazingila..!
Mimi nahisi sio kweli,watapokeaje rushwa waziwazi hivyo? Ni polisi hewa na ishu imetengenezwa ili jeshi la polisi lionekane linachukua hatua dhidi ya maaskari wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…