Serikali: Mteja ana haki ya kuona cheti cha mtoa huduma wa duka la dawa

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Wizara ya Afya kupitia Baraza la Famasi Tanzania itayafungia maduka yote ya dawa ambayo hayajasajiliwa wala kuwa na vibali na kuchukua hatua za kisheria.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Baraza la Famasi Bi.Elizabeth Shekhalage wakati wa ukaguzi unaoendelea nchini kwenye maduka ambayo hayana sifa.

Bi. Shekalaghe amesema kuwa maduka yote ya dawa ambayo hayajasajiliwa na yasiyo na vibali vyenye nembo ya kielekroniki Yaani (barcode Au QR code) yakibainika yatafungwa mara moja na hatua za kisheria zitachukuliwa.

"kwa siku ya jana tumebaini maduka ya dawa 23 ambayo hayajasajiliwa kwa mkoa wa Dar es Salaam na yote tumeyafunga, tunaendelea na zoezi la ukaguzi nchi nzima ili kuweza kubaini maduka yote ya dawa ambayo hayatambuliki na Baraza ". Bi. Shekalaghe

"Vibali vyote vya maduka ya dawa nchini sasa hivi vina nembo ya kielektroniki na tumefanya hivi ili kuweza kuwabaini watoa huduma ambao sio waaminifu".

Hata hivyo Bi. Shekalaghe amewaomba wananchi kutoa taarifa pale ambapo watakuwa na wasiwasi ama kutokuridhika na huduma za dawa wanazozipata kwenye maduka ya dawa ili kuweza kuchukua hatua stahiki

"Tuna namba yetu ambayo unaweza kupiga bila malipo ambayo ni 08 0011 0015, tupigieni ili tuweze kuchukua hatua stahiki kwani kila mwananchi ana haki ya msingi ya kupata huduma ya dawa iliyo sahihi "Amesema

Aidha, amewataka wananchi kuhakikisha wanapoenda kwenye duka la dawa lazima wakute nembo ya duka la dawa muhimu na kuona cheti cha mtoa huduma chenye nembo ya kielektroniki.

Vilevile Bi. Shekalaghe amewaonya watoa huduma kuacha mara moja kutoa huduma za kitabibu katika maduka ya dawa ikiwemo kuchoma sindano na kufanya vipimo. “Si ruhusa kuchoma sindano wala kufanya vipimo vya aina yoyote katika duka la dawa, endapo tukikukamata hatua za kisheria zitachukuliwa "Amesisitiza.

Kwa upande mwingine Bi. Shekalaghe amewasihi watoa huduma na wamiliki wa maduka ya dawa nchini kuwa waaminifu katika utoaji wa huduma za dawa.

"Wamiliki na watoa huduma wengi wa maduka ya dawa sio waaminifu, Hivi karibuni Tumefanya tafiti katika kaguzi zetu tumebaini kuna watoa huduma za dawa ambao wanajifanya wameso
 
Safi sana, na wahudumu waoneshe vyeti vya ufamasia, sio tunahudumiwa na yeyote tu ilimradi anajua dawa na bandage zilipo.

Afya ni issue sensitive.
 
Wamiliki na watoa huduma wengi wa maduka ya dawa sio waaminifu, Hivi karibuni Tumefanya tafiti katika kaguzi zetu tumebaini kuna watoa huduma za dawa ambao wanajifanya wameso
Nyie wenyewe huko jikoni ni waaminifu lakini. Sawa na mama Malaya halafu anao mabinti akawaambia wasifanye umalaya. Niulize hapo ofisini kwako umafia ama ufisadi Mara ngapi umefanya
 
Aisee hii hatar sana, kama mtu anatoa dawa hata haijui watamaliza watu sasa mana wabongo wanavyopenda kwenda Phamarcy Yan mpaka mtu azidiwe ndio anaenda hospital.
Yaani we acha tu
 
Kuna video imenisikitisha sana.View attachment 2197106
hizi certificate za farmacy kutokea hapa na pale ndizo ziliwaponza kampala university kukataliwa udahiri mwaka wa kwanza baada ya wahitimu kuonekana walikiuka sifa za sekondari yaani D nne tena za lazima kwa kemia,biolojia,fizikia na hesabu,naona kwa sasa wamerekebisha.

mtu kmaa huyu unadhani hata kama bado anasoma kama anavyodai itakuwa ni chuo gani maana hata miezi mitatu tu chuo kimachotambulika hawezi fanya upuuzi kama huo,angeishia kuuza panadol na aspirin tu.
 
Hatari sana! Utawakuta wamevaa yake manguo meupe kama wauza Nyama....
kitu nimegundua ni kwamba,hatufi sababu hatunywi mavidonge mengi,ila tunakunywa sana madawa ambayo hayahusiki.
mtu unahisi maumivu ya tumbo,mzigo wa dawa unaopewa mpaka unaogopa.
 
Nyie wenyewe huko jikoni ni waaminifu lakini. Sawa na mama Malaya halafu anao mabinti akawaambia wasifanye umalaya. Niulize hapo ofisini kwako umafia ama ufisadi Mara ngapi umefanya
watu wa farmacy wana watu wao kuanzia wizarani mpaka mahospitali makubwa,kilichopo ni kuuza dawa tu.
 
hizi certificate za farmacy kutokea hapa na pale ndizo ziliwaponza kampala university kukataliwa udahiri mwaka wa kwanza baada ya wahitimu kuonekana walikiuka sifa za sekondari yaani D nne tena za lazima kwa kemia,biolojia,fizikia na hesabu,naona kwa sasa wamerekebisha.

mtu kmaa huyu unadhani hata kama bado anasoma kama anavyodai itakuwa ni chuo gani maana hata miezi mitatu tu chuo kimachotambulika hawezi fanya upuuzi kama huo,angeishia kuuza panadol na aspirin tu.
kuna chuo kinaitwa lugarawa wanadahili wenye D nne,D moja ikiwa ya somo la sayansi wanakuchukua kusoma diploma,nilishangaa sana.
 
Watu waliosomea kozi ya pharmacy wanahasira kwelikweli....ajira mtaani hakuna kwa sababu wengi wao wanataka mishahara mikubwa kwa hiyo wajasiriamali wenye maduka yao wanawakwepa na kuchukua watu wa ( (ADDO) ambao ni cheap.....hata ajira za TAMISEMI NA WIZARA YA AFYA nazo ni chache mnoo haziwatoshi hata kiduchu....FAMASIA KAENI NA WATU WA ADDO MUYAJENGE SISIMIZI HAUWAWI KWA RUNGU NA UKITAKA KULA NA KIPOFU USIMSHIKE MKONO.....
 
Wizara ya Afya kupitia Baraza la Famasi Tanzania itayafungia maduka yote ya dawa ambayo hayajasajiliwa wala kuwa na vibali na kuchukua hatua za kisheria.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Baraza la Famasi Bi.Elizabeth Shekhalage wakati wa ukaguzi unaoendelea nchini kwenye maduka ambayo hayana sifa.
Wanakuja na statement ...."tuta..," watu wameshaumizwa huko wao walikuwa wapi maduka yameota kama uyoga mitaani
 
Wizara ya Afya kupitia Baraza la Famasi Tanzania itayafungia maduka yote ya dawa ambayo hayajasajiliwa wala kuwa na vibali na kuchukua hatua za kisheria.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Baraza la Famasi Bi.Elizabeth Shekhalage wakati wa ukaguzi unaoendelea nchini kwenye maduka ambayo hayana sifa.

Bi. Shekalaghe amesema kuwa maduka yote ya dawa ambayo hayajasajiliwa na yasiyo na vibali vyenye nembo ya kielekroniki Yaani (barcode Au QR code) yakibainika yatafungwa mara moja na hatua za kisheria zitachukuliwa.

"kwa siku ya jana tumebaini maduka ya dawa 23 ambayo hayajasajiliwa kwa mkoa wa Dar es Salaam na yote tumeyafunga, tunaendelea na zoezi la ukaguzi nchi nzima ili kuweza kubaini maduka yote ya dawa ambayo hayatambuliki na Baraza ". Bi. Shekalaghe

"Vibali vyote vya maduka ya dawa nchini sasa hivi vina nembo ya kielektroniki na tumefanya hivi ili kuweza kuwabaini watoa huduma ambao sio waaminifu".

Hata hivyo Bi. Shekalaghe amewaomba wananchi kutoa taarifa pale ambapo watakuwa na wasiwasi ama kutokuridhika na huduma za dawa wanazozipata kwenye maduka ya dawa ili kuweza kuchukua hatua stahiki

"Tuna namba yetu ambayo unaweza kupiga bila malipo ambayo ni 08 0011 0015, tupigieni ili tuweze kuchukua hatua stahiki kwani kila mwananchi ana haki ya msingi ya kupata huduma ya dawa iliyo sahihi "Amesema

Aidha, amewataka wananchi kuhakikisha wanapoenda kwenye duka la dawa lazima wakute nembo ya duka la dawa muhimu na kuona cheti cha mtoa huduma chenye nembo ya kielektroniki.

Vilevile Bi. Shekalaghe amewaonya watoa huduma kuacha mara moja kutoa huduma za kitabibu katika maduka ya dawa ikiwemo kuchoma sindano na kufanya vipimo. “Si ruhusa kuchoma sindano wala kufanya vipimo vya aina yoyote katika duka la dawa, endapo tukikukamata hatua za kisheria zitachukuliwa "Amesisitiza.

Kwa upande mwingine Bi. Shekalaghe amewasihi watoa huduma na wamiliki wa maduka ya dawa nchini kuwa waaminifu katika utoaji wa huduma za dawa.

"Wamiliki na watoa huduma wengi wa maduka ya dawa sio waaminifu, Hivi karibuni Tumefanya tafiti katika kaguzi zetu tumebaini kuna watoa huduma za dawa ambao wanajifanya wameso
Waviweke kwenye maduka yao..

Kwanza hii tabia ya ku admit form four failures kwenye sekta ya Afya ikomeshwe..

Mtu ana D tatu anaenda kufanya nini kwenye afya?
 
Uchafu mwingiii unspita bandarini hamuuoni mnakuja kunyanyasa watu wadogo wadogo vijitawi ilihali shina mnajua lilipo, hongera mama unaupiga mwingi. Katiba mpya lazima sio ombi
 
Back
Top Bottom