Ni hatari sana..
Kuna kila dalili kuwa, baada ya tamko la Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC), vita ya skandali la bandari inakwenda kuchukua sura nyingine kati ya kikundi kilichomo ndani ya serikali kilichotengeneza uchafu huu na Kanisa la Mungu.
Na bila shaka TEC imetangulia tu na muda si mrefu The Christian Council of Tanzania (CCT) na The Council of Pentecostal Churches of Tanzania (CPCT) nao wanakuja na matamko yao na misimamo yao na tunafikiri yatakuwa ni matamko ya namna gani?
Obvious ni kuukataa mkataba huu kwani kwa sababu ziwazo zote, hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu na hajahongwa anaweza kukubaliana na ujinga na uchafu huu unaoitwa IGA kati ya Dubai Emirate na Tanzania.
Kama Rais Samia Suluhu Hassan akishindwa kutumia fursa hii kwa serikali yake kurudi kwenye drawing board ili kufikiria namna sahihi, ya wazi na shirikishi kwa umma ya ubia (partnership) ya uboreshaji wa bandari zetu badala ya njia hii ya mkataba huu mbovu na Dubai kupitia kampuni yao ya DP World, basi awe tayari kuanza kuitumikia hukumu yake yeye na watu wake wote walio nyuma ya scandal hii.
Ni hukumu yake kwa sababu dalili zinaonesha kuwa hiki kikundi baada ya mara ya kwanza kufanikiwa kumshawishi Rais na kwa baraka zake mwenyewe akajiruhusu kujiingiza kwenye shida na aibu hii, basi mission ya kundi hili haijakamilika na linakwenda tena kwake (Rais Samia) na anaweza kutoa baraka zake tena ili kuanzisha vita na kanisa la Mungu wakidhania watafanikisha malengo yao maovu..
Hili likitokea, basi itakuwa ni heri ya wapiganiao haki maana hakuna mamlaka ya serikali yoyote ya kidunia imewahi kushindana na Kanisa la Mungu na mamlaka hiyo ikasimama na kushinda. Tunayo mifano mingi ktk historia ya Biblia kama vile Babeli ya kale, dola la Rumi ya kale, Misri ya Farao nk.
Rais Samia Suluhu Hassan, za kuambiwa changanya na za kwako mama. Wewe ni mwanamke, usiingie ktk historia ya wanawake viongozi wa hovyo waliowahi kuongoza nchi zao na kutoka kwa aibu.