EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Kumekuwa na Kundi kubwa sana la wananchi wakisota Rumande kwa kile kinachotajwa kuwa "UPELELEZI HAUJAKAMILIKA" hii kitu imekuwa adui mkubwa sana wa haki za watuhumiwa.
Kuna jamaa flani hapa mtaani amekaa rumande/jela kwa miaka miwili kwa kesi ya uhujumu uchumi, alikuwa mtuhumiwa namba mbili, kufuatilia polisi wanasema wameshamaliza upelelezi mwaka jana ila file lipo kwa DPP, kesi inatajwa mahakamani na kuahirishwa kila mara.
Kuna watu wapo "ndani" 10+ yrs kwa kisingizio cha upelelezi.
Kesi ya kubaka mwanamke mwathirika akishaoga tu ushahidi umeisha unachunguza nini miaka na miaka
Kwa style hii DPP amekua kikwazo kikubwa sana cha haki kutendeka.
Hapo huzazungumzia maamuzi mabovu ya mahakimu yanayoelekea kuupendelea "kuhimili uliojichimbia chini zaidi" wakitarajia kulipwa fadhila kwa kuteuliwa UJAJI.
Muhimili wenye kina kirefu ndio unaopanda aina ya hukumu inawafaa watuhumiwa hasa wanasiasa rejea wanachama wa CCM wanaotuhumiwa kutoa rushwa hapo husikii TAKUKURU wakijinasibu kuwaweka ndani licha ya kuwepo kwa clips zao. Tuje kwa mtoto wa Lowasa, Ndugu wa Rostam Aziz, Mbunge wa Siha alikuwa na kesi ya kufoji kitambulisho ya TISS
mambo ni mengi ila ndio hivyo......
""tumipenda wenyewe, chaguo letu wenyewe, na wavimbe wapasuke,
Wacha tuisome namba.""
nawasilisha