Serikali na sekta binafsi kuanzisha vituo vya kukodisha mitambo ya uchimbaji madini

Serikali na sekta binafsi kuanzisha vituo vya kukodisha mitambo ya uchimbaji madini

Wizara ya Madini

Govt Institution
Joined
Apr 12, 2025
Posts
50
Reaction score
20
Serikali kwa ushirikiano na sekta binafsi imejipanga kuanzisha vituo vya ukodishaji mitambo ya uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kufanya shughuli zao kwa tija.
IMG-20250606-WA0304.jpg


Hayo yamesemwa leo tarehe 06 Juni, 2025 na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde (Mb) wakati akihitimisha Kongamano la Maonesho ya Madini mkoani Mara kwenye viwanja vya Mukendo vilivyopo Manispaa ya Musoma.

"Sote tunatambua kwamba wachimbaji wadogo hawana uwezo wa kununua na kuihudumia mitambo ya kisasa kama kwa ajili ya uchimbaji.
IMG-20250606-WA0310.jpg


Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza Wizara ya Madini kuja na mpango huu ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata fursa ya kutumia teknolojia ya kisasa kwenye shughuli zao lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa madini.

Sambamba na Mitambo ya kukodisha tunatarajia pia kuanzisha Kituo cha Elimu ya Uchenjuaji wa madini ambacho kitakuwa na Mtambo wa Uchenjuaji wa madini eneo la Nyamongo-Tarime.
IMG-20250606-WA0303.jpg


Ni matarajio yetu sasa kwamba mpango huu unakwenda kubadilisha uchumi wa wachimbaji wadogo kwa kuinua vipato vyao na hatimaye kuongeza mchango zaidi kwenye ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na sekta ya Madini”Alisema Mavunde

Awali, akisoma taarifa ya sekta ya madini kwa Mkoa wa Mara, Mhandisi Amin Msuya alisema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Mhe. Rais, Mkoa wa Mara umezalisha dhahabu tani 58.90 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 6.90 kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa.
IMG-20250606-WA0308.jpg

Akitoa salamu za wachimbaji, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania, Bw. John Wambura Bina amempongeza Mh. Rais Samia S. Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye sekta ya madini na kutoa rai kwa wachimbaji wadogo kuchangamkia fursa zilizopo Mkoani Mara na kuwahimiza kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa kwani Serikali imeziboresha ili kulinda maslahi ya wachimbaji wadogo nchini.
IMG-20250606-WA0309.jpg


Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Kanali Evans Mtambi alieleza kwamba lengo la kongamano hilo ni kuleta pamoja wadau wa sekta kujadili fursa zilizopo mkoani Mara na namna ya kuzifikia. Aidha, alisisitiza kuwa kongamano hili litaendelea kufanyika kila mwaka ili liwe chachu ya kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye GDP ya Mkoa ambao kwa sasa umefikia asilimia 18.
IMG-20250606-WA0307.jpg
 

Attachments

  • IMG-20250606-WA0310.jpg
    IMG-20250606-WA0310.jpg
    212.7 KB · Views: 28
No REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION NO REFORM NO ELECTION
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Serikali kwa ushirikiano na sekta binafsi imejipanga kuanzisha vituo vya ukodishaji mitambo ya uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kufanya shughuli zao kwa tija.View attachment 3359726

Hayo yamesemwa leo tarehe 06 Juni, 2025 na Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde (Mb) wakati akihitimisha Kongamano la Maonesho ya Madini mkoani Mara kwenye viwanja vya Mukendo vilivyopo Manispaa ya Musoma.

"Sote tunatambua kwamba wachimbaji wadogo hawana uwezo wa kununua na kuihudumia mitambo ya kisasa kama kwa ajili ya uchimbaji. View attachment 3359728

Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza Wizara ya Madini kuja na mpango huu ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata fursa ya kutumia teknolojia ya kisasa kwenye shughuli zao lengo la kuongeza tija na uzalishaji wa madini.

Sambamba na Mitambo ya kukodisha tunatarajia pia kuanzisha Kituo cha Elimu ya Uchenjuaji wa madini ambacho kitakuwa na Mtambo wa Uchenjuaji wa madini eneo la Nyamongo-Tarime.View attachment 3359729

Ni matarajio yetu sasa kwamba mpango huu unakwenda kubadilisha uchumi wa wachimbaji wadogo kwa kuinua vipato vyao na hatimaye kuongeza mchango zaidi kwenye ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na sekta ya Madini”Alisema Mavunde

Awali, akisoma taarifa ya sekta ya madini kwa Mkoa wa Mara, Mhandisi Amin Msuya alisema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Mhe. Rais, Mkoa wa Mara umezalisha dhahabu tani 58.90 zenye thamani ya Shilingi Trilioni 6.90 kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa.
View attachment 3359730
Akitoa salamu za wachimbaji, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania, Bw. John Wambura Bina amempongeza Mh. Rais Samia S. Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya kwenye sekta ya madini na kutoa rai kwa wachimbaji wadogo kuchangamkia fursa zilizopo Mkoani Mara na kuwahimiza kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa kwani Serikali imeziboresha ili kulinda maslahi ya wachimbaji wadogo nchini.View attachment 3359734

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mh. Kanali Evans Mtambi alieleza kwamba lengo la kongamano hilo ni kuleta pamoja wadau wa sekta kujadili fursa zilizopo mkoani Mara na namna ya kuzifikia. Aidha, alisisitiza kuwa kongamano hili litaendelea kufanyika kila mwaka ili liwe chachu ya kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye GDP ya Mkoa ambao kwa sasa umefikia asilimia 18.View attachment 3359736
Vipi nyie mtakuwa mnajibu hoja za wadau au mtakuwa mnapiga kimya kama wenzenu wa TANESCO na TRA Tanzania ?
 
Back
Top Bottom