#COVID19 Serikali na siasa za Corona, yanayosemwa sio yanayofanyika

#COVID19 Serikali na siasa za Corona, yanayosemwa sio yanayofanyika

Wote ni mashuhuda kwa jinsi serikali ilivyojipambanua kukabiliana na janga la corona, na hii imepelekea wengi kupongeza hatua ambazo serikali imepanga/ilipanga kuzichukua.

Serikali imeweka mkazo mkubwa sana ili kulinda watu wake dhidi ya corona na ndio maana matamko mengi yametolewa na wakuu wa mikoa ili kukabiliana na hili suala.

Mkuu wa mkoa dar alisema daladala ziwe level seat, watu wote wavae barakoa na mikusanyiko hairuhusiwi.

Ni ukweli usiopingika kuwa corona inaua na imeua ndugu zetu wengi na bado inaendelea kuua.

Hivyo hatua hizi za mkuu wa mkoa Amos Makalla zipo sahihi Sana, lakini kwa nini hazisimamii?

Tatizo lipo hapo, matamko ya kila namna katoa kuhusu corona na mikusanyiko, lakini amekuwa ndio wa kwanza kuvunja kule nacho yeye mwenyewe aliagiza.
Au corona imeisha? Kama ni hivyo basi watu waambiwe, na Kama corona bado ipo mbona mnashindwa kusimamia maagizo yenu?

Jana mkuu wa mkoa alikuwa kwenye mkusanyiko huko wa ndondo cup, huku uwanja ukifurika bila watu kuchukua tahadhari zozote.

Leo tena uwanja wa taifa umefurika, hakuna social distancing Wala barakoa. Lakini mkuu wa mkoa yupo kimya kama haoni vile

Kama Jambo ni gumu kulitekeleza, serikali msiwe mnatoa matamko.
View attachment 1914861View attachment 1914862View attachment 1914864View attachment 1914867
Ccm hawaeleweki, vyama vya upnzani vikitaka kufanya mikutano hata ya ndani tu vinazuiwa eti korona,sasa hii korona ipo upande wa upinzani tu?
 
Kama hivi
7be36de4511800ead8fed7eb809b3792.jpg
 
Corona haitaki kukaa Tanzania wanalazimisha,mwishowe inaanza kuwaaibisha tu.
Imenuna haitaki kuchukua mtu.
 
Mkuu vipi tena? lengo si lilikuwa kuungana tu na 'wenzetu' na kuitangazia dunia tu kwamba na sisi tunae uviko ili twende sawa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Viongozi wenyewe wanavaa barakoa kama wakiwa wanakutana na viongozi wa kimataifa sasa. Itakuaje sisi wananchi
 
Back
Top Bottom