Serikali na TFF ichukue Hatua ya kuwadhibiti hawa Wassmaji wa Vilabu

Zakayomfupi

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2024
Posts
1,040
Reaction score
1,002
Nimepitia maoni ya watu wengi kuhusiana na hawa wasemaji wa vilabu. Wengi wao hawana weledi. Angalia namna msemaji wa Simba alivyokua akimuongelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, juzi Kamwe kamtolea maneno ya hovyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kashfa na kumshambulia binafsi. Wasemaji sasa wanaweza kuwatweza viongozi wa juu wa serikali na watu wapuuzi wakiwashangilia. Nao wanajiona wakubwa kuliko viongozi, wanaona aliye juu yao ni Mh. Rais pekee. Serikali na TFF ichukue hatua haraka kuwakata mikia iliyoanza kuwaota hawa wasemaji.
 
Wasemaji hawana weledi je hao wakuu wa mikoa nao wana weledi? Au ndio mkubwa hakosei? Hao wakuu wa mikoa wanajiingiza kwenye ushabiki
 
Umeamka asubuhi umeshibia magimbi unaandika vitu havieleweki.
Wakuu wa mkoa wanahusikaje na mpira?.
 
Wasemaji hawana weledi je hao wakuu wa mikoa nao wana weledi? Au ndio mkubwa hakosei? Hao wakuu wa mikoa wanajiingiza kwenye ushabiki
Alichokifanya Kamwe ni kumshambulia mkuu wa Mkoa binafsi. Unawezaje kukejeli imani ya wenzetu wasabato?
 
Nimepitia maoni ya watu wengi kuhusiana na hawa wasemaji wa vilabu. Wengi wao hawana weledi. Angalia namna msemaji wa Simba alivyokua akimuongelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, juzi Kamwe kamtolea maneno ya hovyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kashfa na kumshambulia binafsi. Wasemaji sasa wanaweza kuwatweza viongozi wa juu wa serikali na watu wapuuzi wakiwashangilia. Nao wanajiona wakubwa kuliko viongozi, wanaona aliye juu yao ni Mh. Rais pekee. Serikali na TFF ichukue hatua haraka kuwakata mikia iliyoanza kuwaota hawa wasemaji.
Ngoja wamtukane na Kabudi labda serikali itaamka usongizini. Mi niliachaga kushabikia hizi timu Yanga na Simba baada ya kuona ni kundi la wapumbavu. Wana kiburi kwani nyuma yao kuna viongozi wakubwa mpk marais. Ligi yetu bila Simba na Yanga kupangiwa ligi zao haiendi popote. Club gani kuanzia mvuta bangi mpk Rais wa nchi ni mshabiki tena waziwazi. Wametuharibia mpira wetu hao wapuuzi.
 
Nimepitia maoni ya watu wengi kuhusiana na hawa wasemaji wa vilabu. Wengi wao hawana weledi. Angalia namna msemaji wa Simba alivyokua akimuongelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, juzi Kamwe kamtolea maneno ya hovyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora, kashfa na kumshambulia binafsi. Wasemaji sasa wanaweza kuwatweza viongozi wa juu wa serikali na watu wapuuzi wakiwashangilia. Nao wanajiona wakubwa kuliko viongozi, wanaona aliye juu yao ni Mh. Rais pekee. Serikali na TFF ichukue hatua haraka kuwakata mikia iliyoanza kuwaota hawa wasemaji.
Iwapo kolo kasemwa na mwananchi je?
 
Alichokifanya Kamwe ni kumshambulia mkuu wa Mkoa binafsi. Unawezaje kukejeli imani ya wenzetu wasabato?
Kwahiyo unaona ni sawa mkuu wa mkoa kutumia mamlaka yake kuchafua brand za watu? Anatoa tuhuma za rushwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari wakati TAKUKURU ipo chini yake na anauwezo wa kuwaagiza wafanye kazi yao badala ya kulia lia hovyo.
 
tungefanya kama kwa wenzetu duniani, Coach/Manager ndo Msemaji wa Timu. Tungebaki tumazungumza Football only
 
Kazi za mkuu wa mkoa sio kuwa sehemu ya mambo ya mpira.... Serikali hamlipi kuwa msemaji wa timu... Wqnachofananya wakuu wa mikoa ni kuingia kwenye mapambano yasiyowahusu hivyo wakipewa za uso wasitegemee msaada wa serikali....!!!. Alichokifanya mkuu wa mkoa juzi ni upuuzi na Ali Kamwe alikuwa sahihi 100% kumpa za uso.... Mkuu wa mkoa unatoa shutuma za kipumbavu kiasi kile..... Kama mtendaji mkuu wa mkoa alichukua hatua gani kama yanga walihusika na rushwa?. Ni mpumbavu na Alli alimstahi kwa kauli nyepesi zile.
 
Back
Top Bottom