Serikali na TRA wekeni utaratibu wa kupata Kodi ya bodaboda

Hii mie nashauri wapewe kitu Kama leseni so wawe wanazilipia wanatambulika na Kila boda awe na namba iandikwe kwa boda yake, hii leseni akilipia 25-50k kwa mwaka sio mbaya. Yaani awe na leseni na atambulike ili hata Kama kambeba mtu hawafahamiani mtu anaweza akachukua namba yake
Una bonge la hoja
Serikali ilitumie wazo lako na ikulipe pesa nyingi
 
Ingekuwa hizo Kodi zinaenda kwenye matumizi sahihi baada ya kukusanywa hata Mimi ningeshikia bango hili wazo lako, Tena ningependekeza walipe hata 50,000/= Kwa mwaka.

Ila Kwa sababu Hela ya Kodi yenyewe Huwa inaishia kwenye mambo ya kipumbavu kama vile Abdul kuwahonga wapinzani, kununua maV8 kila mwaka, kulipana posho za ovyo ovyo, sijui goli la mama... Nawashauir hao boda boda wasilpe kabisa hata 100, na nnawahasa na watanzania wengine wakipata mwanya wa kukwepa Kodi wasilipe, maana hata wakilipa hiyo Hela haiendi kwenye makusudio husika zaidi ya kuwaneemesha tu mafisadi.
 
Bodaboda ni sekta rasmi Kwa Sasa.
Ni dharau kubwa Kwa bodaboda ambao kwasasa wapo zaidi ya watu million 10 hawa watu wote kila mtu akilipa elfu 10 Kwa mwaka ni pesa ndefu

Kulipa Kodi ni jukumu la kila anayeingiza kipato

Kama serikali inatoza Kodi mlinzi wa SUMA JKT, mwalimu, police, nurse n. K sio haki kumpotezea bodaboda anayeingiza zaidi ya elfu 30,000 Kwa siku

Hawa bodaboda wamekuwa ni waharibufu wa miundo yetu ya barabarani kwakuwa hawana uchungu nayo maana hawashiriki kuijenga Kwakuwa hawapi kodi

Hawa bodaboda walevi na fujo zao hawashindwi kulipa Elfu 10 Kwa mwaka ilihali kila siku wanalewa pombe, bangi,na ugolo

Mh Mwigulu ingia ofsini na wataalam wako wa Kodi mpate kuvuna pesa kutoka Kwa hawa bodaboda

Pesa ikipatikana irudi kwenye maendeleo watu tuyaone, siyo mkanunue timu za mipira na kuhonga wapinzani
Ni rahisi sana sema Tatizo wafanyakazi wa umma sio wabunifu
 
Ingekuwa hizo Kodi zinaenda kwenye matumizi sahihi baada ya kukusanywa hata Mimi ningeshikia bango hili wazo lako, Tena ningependekeza walipe hata 50,000/= Kwa mwaka.

Ila Kwa sababu Hela ya Kodi yenyewe Huwa inaishia kwenye mambo ya kipumbavu kama vile Abdul kuwahonga wapinzani, kununua maV8 kila mwaka, kulipana posho za ovyo ovyo, sijui goli la mama... Nawashauir hao boda boda wasilpe kabisa hata 100, na nnawahasa na watanzania wengine wakipata mwanya wa kukwepa Kodi wasilipe, maana hata wakilipa hiyo Hela haiendi kwenye makusudio husika zaidi ya kuwaneemesha tu mafisadi.
Tuhimizane kulipa kodi
 
Tuhimizane kulipa kodi
Hakuna Mtanzania ambaye halipi Kodi..., bali kuna watu wanafuja hizo Kodi (Jasho la Mlipa Kodi) na mbaya zaidi wanachukua mpaka mbegu

Bodaboda ni sekta rasmi Kwa Sasa.
Ni dharau kubwa Kwa bodaboda ambao kwasasa wapo zaidi ya watu million 10 hawa watu wote kila mtu akilipa elfu 10 Kwa mwaka ni pesa ndefu

Kulipa Kodi ni jukumu la kila anayeingiza kipato

Kama serikali inatoza Kodi mlinzi wa SUMA JKT, mwalimu, police, nurse n. K sio haki kumpotezea bodaboda anayeingiza zaidi ya elfu 30,000 Kwa siku

Hawa bodaboda wamekuwa ni waharibufu wa miundo yetu ya barabarani kwakuwa hawana uchungu nayo maana hawashiriki kuijenga Kwakuwa hawapi kodi

Hawa bodaboda walevi na fujo zao hawashindwi kulipa Elfu 10 Kwa mwaka ilihali kila siku wanalewa pombe, bangi,na ugolo

Mh Mwigulu ingia ofsini na wataalam wako wa Kodi mpate kuvuna pesa kutoka Kwa hawa bodaboda

Pesa ikipatikana irudi kwenye maendeleo watu tuyaone, siyo mkanunue timu za mipira na kuhonga wapinzani
Kwamba kila watu 6 nchi hii kuna Bodaboda mmoja? Hata milioni hawafiki hao.
 
Wanalipa Kodi indirect Kwa kununua mafuta,pamoja na vifaa vinavyoharibika kwenye bodaboda zao.labda ungesema viongozi ambao hawalipi Kodi kama rais,waziri mkuu,makamu na baadhi ya wakuu wa taasisi waanze kulipa Kodi.Maana Hawa tunawagharamia Kwa pesa nyingi sana.mfano gari Moja tu la rais au makamu linagharimu milioni Miatano ambalo linakula mafuta Kila siku si chini ya milioni Moja Bado matengenezo na hizo zote tunazilipia sisi wtz wanyonge
 
Umeongea point sana. Umeongea kile wafanyabiashara tunachowaambia kila mara TRA. Watanue wigo wa Kodi sio kama hivi kila mara ni kugombana na mtu ksbb tu ana duka,basi kila wakati anaongezewa Kodi huyu mwenye duka tu.
Hata Magu aliwahi kuwahoji TRA mmeaminiwa kukusanya kodi,lakini mnashindwaje kuongeza vyanzo vipya vya Kodi?.

Sasa kama huyu bodaboda,wanatengeneza hela nzuri sana wanashindwaje kuingizwa kwenye kulipa Kodi miaka yote hii?. Tena kama ulivyoongea bodaboda ni waharibifu wakubwa wa miundombinu ya barabara kuliko hata mwenye kiduka.

Sijui nani TRA aliwadanganya kwamba ukifungua duka tu tayari umekosea,TRA wana wewe tu? Wanapelekeshwa watu mpaka wanafunga biashara.
Isiwe elfu 10. Waanzie na elfu 50 kwa mwaka. Kwa kipato chao elfu 50 kwa mwaka ni bure kabisa. Waanze nao kwa elfu 50 kwa mwaka.
Kama sikosei nadhani sheria ipo na wanalipa 65,000/=. Kitu cha kufahamu hapa nacholewa tra wao hawawezi lipisha kodi bila kufata sheria , wao wanasimamia sheria ili kuweza kukusanya kodi hizo. Kuhusu kuongeza wigo ni kwamba wanatakiwa kufahamu wale wote waliopo kwenye sheria ya kulipa kodi wanalipa kulingana na ukubwa wao kama ilivyo kwenye sheria. Hawawezi kukusanya kodi kwa wafanyabiashara ambao hawapo kwenye sheria. mfano mwanzo boda walikuwa hawapo sasa hivi nachojua ni 65,000/= kwa mwaka ndiyo sheria ilipita hivo mwaka juzi.
 
Hiyo sheria sijaiona
 
Hawawezi kulipa hio Kodi Kama wako milioni 10 Hilo NI jeshi kubwa...kulipa Kodi tu kutawafanya wajitambue wanasiasa watapata mkwamo kuwatumia... Watapata shida kuwashawishi...hata wangerudisha ya kichwa hayo mabango ya Samia what yangeshapigiwa kelele...misafara ya hovyo ingepigiwa kelele..
 
Tena hiyo Kodi iingizwe kwenye Mfumo rasimi wa kulipia laki moja kwa mwaka ili kama itaonekana kubwa waachane na bodaboda wakalime tuinue uchumi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwafanya vijana wafikirie nje ya box. Hongera mleta mada
 
Nadhani zipo Kodi za vyombo za Moto zilihamishiwa kwenye mafuta na pia wanaponunua mafuta mara kwa mara pia ipo kodi ndani yake pia chombo hutozwa Kodi wakati was usajili, tayari no walipa Kodi labda hoja iwe kuwaongezea kiwango Cha ulipaji.
 
Tena hiyo Kodi iingizwe kwenye Mfumo rasimi wa kulipia laki moja kwa mwaka ili kama itaonekana kubwa waachane na bodaboda wakalime tuinue uchumi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwafanya vijana wafikirie nje ya box. Hongera mleta mada
Una hoja nzuri mno mkuu
 
Back
Top Bottom