Serikali na TRA wekeni utaratibu wa kupata Kodi ya bodaboda

Una bonge la hoja
Serikali ilitumie wazo lako na ikulipe pesa nyingi
 
Ingekuwa hizo Kodi zinaenda kwenye matumizi sahihi baada ya kukusanywa hata Mimi ningeshikia bango hili wazo lako, Tena ningependekeza walipe hata 50,000/= Kwa mwaka.

Ila Kwa sababu Hela ya Kodi yenyewe Huwa inaishia kwenye mambo ya kipumbavu kama vile Abdul kuwahonga wapinzani, kununua maV8 kila mwaka, kulipana posho za ovyo ovyo, sijui goli la mama... Nawashauir hao boda boda wasilpe kabisa hata 100, na nnawahasa na watanzania wengine wakipata mwanya wa kukwepa Kodi wasilipe, maana hata wakilipa hiyo Hela haiendi kwenye makusudio husika zaidi ya kuwaneemesha tu mafisadi.
 
Ni rahisi sana sema Tatizo wafanyakazi wa umma sio wabunifu
 

 
Tuhimizane kulipa kodi
 
Tuhimizane kulipa kodi
Hakuna Mtanzania ambaye halipi Kodi..., bali kuna watu wanafuja hizo Kodi (Jasho la Mlipa Kodi) na mbaya zaidi wanachukua mpaka mbegu

 
Kwamba kila watu 6 nchi hii kuna Bodaboda mmoja? Hata milioni hawafiki hao.
 
Wanalipa Kodi indirect Kwa kununua mafuta,pamoja na vifaa vinavyoharibika kwenye bodaboda zao.labda ungesema viongozi ambao hawalipi Kodi kama rais,waziri mkuu,makamu na baadhi ya wakuu wa taasisi waanze kulipa Kodi.Maana Hawa tunawagharamia Kwa pesa nyingi sana.mfano gari Moja tu la rais au makamu linagharimu milioni Miatano ambalo linakula mafuta Kila siku si chini ya milioni Moja Bado matengenezo na hizo zote tunazilipia sisi wtz wanyonge
 
Kama sikosei nadhani sheria ipo na wanalipa 65,000/=. Kitu cha kufahamu hapa nacholewa tra wao hawawezi lipisha kodi bila kufata sheria , wao wanasimamia sheria ili kuweza kukusanya kodi hizo. Kuhusu kuongeza wigo ni kwamba wanatakiwa kufahamu wale wote waliopo kwenye sheria ya kulipa kodi wanalipa kulingana na ukubwa wao kama ilivyo kwenye sheria. Hawawezi kukusanya kodi kwa wafanyabiashara ambao hawapo kwenye sheria. mfano mwanzo boda walikuwa hawapo sasa hivi nachojua ni 65,000/= kwa mwaka ndiyo sheria ilipita hivo mwaka juzi.
 
Hiyo sheria sijaiona
 
Hawawezi kulipa hio Kodi Kama wako milioni 10 Hilo NI jeshi kubwa...kulipa Kodi tu kutawafanya wajitambue wanasiasa watapata mkwamo kuwatumia... Watapata shida kuwashawishi...hata wangerudisha ya kichwa hayo mabango ya Samia what yangeshapigiwa kelele...misafara ya hovyo ingepigiwa kelele..
 
Tena hiyo Kodi iingizwe kwenye Mfumo rasimi wa kulipia laki moja kwa mwaka ili kama itaonekana kubwa waachane na bodaboda wakalime tuinue uchumi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwafanya vijana wafikirie nje ya box. Hongera mleta mada
 
Nadhani zipo Kodi za vyombo za Moto zilihamishiwa kwenye mafuta na pia wanaponunua mafuta mara kwa mara pia ipo kodi ndani yake pia chombo hutozwa Kodi wakati was usajili, tayari no walipa Kodi labda hoja iwe kuwaongezea kiwango Cha ulipaji.
 
Tena hiyo Kodi iingizwe kwenye Mfumo rasimi wa kulipia laki moja kwa mwaka ili kama itaonekana kubwa waachane na bodaboda wakalime tuinue uchumi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwafanya vijana wafikirie nje ya box. Hongera mleta mada
Una hoja nzuri mno mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…