Serikali na Tume ya Warioba walichokisema juu ya Katiba Mpya

Serikali na Tume ya Warioba walichokisema juu ya Katiba Mpya

Counsel Jr

New Member
Joined
Jan 27, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Habari wanajukwaa na Watanzania wote kwa ujumla? Nachukua fursa hii adimu kwanza kumshukuru Mungu wa rehema!

Niende kwenye mada moja kwa moja, kwa muda sasa Tanzania tuliingia katika mchakato wa Katiba mpya jambo ambalo mpaka leo halijazaa matunda siyo kwasababu pengine wahusika wa jambo hili (Serikali na Tume ) hawakuona umuhimu wake kwani mchakato ushaanza bali pengine waliona wameruka hatua ndio maana mpaka leo haujakamilika.

Hapa hatua ninayomaanisha ni hatua ya kuwajuza kwanza Katiba tuliyonayo (Katiba ya 1977 kama ambavyo imekuwa ikifanyiwa mabadiliko) inaongelea nini, kuwafanya Watanzania wanaielewa kwa undani katiba ya 1977 ili waweze kufanya maamuzi sahihi kipindi wanaipigia kura na bunge maalumu la katiba kuipitisha. Ibara ya 8 ya Katiba ya 1977 inasema bayana kuwa katiba inatokana na nguvu ya raia, kwahiyo Watanzania ndio wanaopaswa kuwa wadau wakubwa wa sheria hii mama.

Kwahiyo nafikiri kwa hili, serikali pamoja na tume ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Warioba walikosea na nafikiri ndiyo maana mpaka muda huu hatujafikia lengo hilo, hivyo basi:
Kupitia wadau mbalimbali, serikali iweke utaratibu wa kuhakikisha Watanzania wanaijua katiba ya 1977 ili kuwaruhusu hata wakiwa wanaipigia kura Katiba mpya ili ipite wawe wanajua uimara na udhaifu wa Katiba ya 1977 na kufanya wanakuwa na wigo mpana wa kufanya maamuzi.

Binafsi mambo ninayoyapendekeza na kuishauri serikali kupitia wizara ya Katiba na Sheria, wawahusishe wadau kama vile Mashirika ya kijamii yale ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali, lakini pia serikali ivihusishe vyombo ya habari kama vile Televisheni na Redio kutoa elimu juu ya Katiba ya 1977-sura baada ya sura, sehemu baada ya sehemu, ibara baada ya ibara hata kwa muda wa miezi sita tutakuwa tumefanikiwa pakubwa.
Lakini pia kuna mitandao ya kijamii kupitia kurasa zinazoaminika kama vile Jamiiforums kuanzisha utaratibu wa kuchambua katiba ili jamii ya Watanzania iweze kuielewa.

Mwisho kabisa, nina uhakika ukiwekwa utaratibu kupitia wadau (mashirika, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari) kwa muda wa miezi sita tu, angalau 75% ya Watanzania watakuwa wameielewa vizuri katiba yetu na watakuwa na uwezo kung'amua juu ya musakhbari wa Katiba mpya.

NCHI YENYE MAENDELEO NA UCHUMI IMARA HUTEGEMEA UIMARA WA SHERIA ZAKE.... NAOMBA TULIUNGE MKONO HILI!!!
 
Back
Top Bottom