Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
Kama kweli ikiiwa tunataka nchi yetu Ipige hatua, ni vyema kila changamoto inayojitokeza, tuione kama fursa ya kutufikisha pahala!
JPM ingawa hatumpendi, lakini wakati wa Covd 19, yeye aliona kuwa ni fursa, wakati mataifa mengine wakijilockdawon, yeye alihimiza wananchi kuchapa kazi, na mwisho wa siku nchi ikawa kwenye uchumi wa kati, katikati ya dholuba kali, yeye akawajaza wananchi matumaini kuwa, tutavuka!
Naheshimu kada ya wasomi kwa sababu wasomi, ikiwa wataamua kutumia vema taaluma zao, nchi itasogea, lakini pia wasomi wakilala, na nchi inalala, Je sasa wasomi mko usingizini?
Kipindi cha nyuma sana, sikumbuki ni lini, ila nakumbuka tukio moja katika nchi ya China,
Nchini China, hakuna nishati ya mafuta, miaka hiyo kuliibuka mgogoro Mkubwa wa nishati na kupanda sana kwa nishati hiyo ya mafuta kama ilivyo leo!
Kipindi hicho, China ndio ilikuwa kwenye harakati zake za kuujenga uchumi wake, na penye nia pana njia,
Wasomi na viongozi wa nchi hiyo walikaa kwa pamoja ili kutafuta mwarobaini wa kupanda nishati ya Mafuta na nini kama nchi wafanye ili nishati hiyo isiwe sababu ya nchi hiyo kupaa kiuchumi
Wazo walilolibuni! kwa nchi kama ya Tanzania, ni matusi kwa wengi hasa watembelea V8, serikali yake iliamua kuwagawia wafanyakazi wake wote Baiskeli! usafiri ulioruhusiwa kubaki barabarani ni umma pekee, kwa atakaye taka usafiri wa gari, basi atatumia daldala, ili tu harakati za kuivusha nchi yao kuelekea uchumi Mkubwa usikwame
Nikirudi ktk hoja yangu, kwanza Mimi niseme kuwa, ni RAIA wa kawaida kabisa na elimu yangu ni ya kuungaunga! Kwetu sisi wakulima, wakati huu wa ukame na kupanda kwa gharama za maisha, nadhani serikali ndo ingesimama na wakulima hasa kilimo cha umwagiliaji, serikali iwawezeshe na bajeti yake iongezwe na isimamiwe na watu watu kweli,!
Au serikali pamoja na wasomi wetu, mnatumiaje maarifa yenu ambayo serikali inawalipa kwayo?
Mgogoro wa mafuta na kupanda kwa bidhaa zote nchini, mnafanya nini ili iwe ni fursa katika nchi yetu au mnawaza kupandishiana posho tuu lakini ni kipi mnafanya ni hata hakijulikani!
Imekuwa kila mmoja Analia, si msomi na hata wasiosoma, wote wanalalamika, Je, ni Nani sasa anayesimama katikati yetu kusolve matatizo ya wananchi hasa katika kupanda kwa gharama za maisha??