Serikali naomba mtofautishe muonekano wa sarafu za shilingi 500 na shilingi 10.

Serikali naomba mtofautishe muonekano wa sarafu za shilingi 500 na shilingi 10.

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Hizi sarafu mbili zinafanana mno, kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa mtu kuzitofautisha haraka haraka hasa katika mazingira yenye giza. Mfano jana usiku nisingekuwa makini ilikuwa nishikishwe sarafu 6 za shillingi 10 nikidhani ni elfu 3.

Serikali fanyeni kitu kuzitofautisha hizi sarafu kimuonekano.
 
Kwani sarafu za shillingi10 zipo kwenye mzunguko?
 
Siku hizi sarafu ya mwisho inayotumika kwenye mzunguko ni 50. Hizi 10 umetumia wapi au zinatumika tu kufanya utapeli?
 
Siku hizi sarafu ya mwisho inayotumika kwenye mzunguko ni 50. Hizi 10 umetumia wapi au zinatumika tu kufanya utapeli?
Siku hizi tangu lini? Bank of Tanzania haijawahi toa statement kuondoa sarafu yoyote kwenye mzunguko. Hazitengenezwi mpya ila hazijazuiwa kutumika
 
Umetumia wapi sarafu ya shilingi kumi au ni ubishiubishi wa chadema tuh
 
Siku hizi tangu lini? Bank of Tanzania haijawahi toa statement kuondoa sarafu yoyote kwenye mzunguko. Hazitengenezwi mpya ila hazijazuiwa kutumika
Hebu zitafute hizo uwe nazo hata za elfu kumi tu halafu nenda nazo popote kafanyie matumizi yako.
 
Hebu zitafute hizo uwe nazo hata za elfu kumi tu halafu nenda nazo popote kafanyie matumizi yako.
Huko ndio kuzuiliwa? Nitafute sarafu za shilingi 10 zitimie shilingi 10,000 nina kichaa? Kwani note ya 10,000 sina
 
Back
Top Bottom