Serikali nyingi na chache ukweli ni upi

Sungurampole

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2007
Posts
984
Reaction score
205
Malumbano haya yanapamba moto, ila mantiki haipewi nafasi. wako wanaosema kuwa hawaoni tatizo la pendekezo la rasimu kuwa serikali ziwe ziwe serikali tatu. sioni tatizo la gharama linakujaje, kwani ukubwa wa serikali na gharama ni uamuzi wetu ambao utategemea uwezo. Pia hakuna gharama zinazoendana na idadi ya serikali kwamba gharama ya serikali moja ni x hivyo zikiwa tatu ni 3x zikiwa mbili ni 2x. Na kama zipo na tunafikiri na gharama tumeamua iwe kigezo cha msingi basi jibu ni wazi kuwa tuwe na serikali moja na siyo mbili wala tatu. Kwa upande mwingine wako wanaosema kuwa na serikali tatu kutaua Muungano, huenda ni kweli lakini kama msingi mkuu wa kuchagua idadi ya serikali ni kuulinda Muungano basi suluhisho ni kuwa na serikali moja.

Nasema hivyo kwani hizi mbili za sasa zimetumika nguvu nyingi na hata wakati mwingine unaweza kusema hila, ulaghai au mabavu ili kuzifanye ziwepo huku tuendako hazitatufaa.
 
Kama ndoa ya muungano imeshindikana Tuachane kwa wema,.tusisumbue watoto kwaajili ya mapungufu ya ndoa,.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…