Sungurampole
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 984
- 205
Malumbano haya yanapamba moto, ila mantiki haipewi nafasi. wako wanaosema kuwa hawaoni tatizo la pendekezo la rasimu kuwa serikali ziwe ziwe serikali tatu. sioni tatizo la gharama linakujaje, kwani ukubwa wa serikali na gharama ni uamuzi wetu ambao utategemea uwezo. Pia hakuna gharama zinazoendana na idadi ya serikali kwamba gharama ya serikali moja ni x hivyo zikiwa tatu ni 3x zikiwa mbili ni 2x. Na kama zipo na tunafikiri na gharama tumeamua iwe kigezo cha msingi basi jibu ni wazi kuwa tuwe na serikali moja na siyo mbili wala tatu. Kwa upande mwingine wako wanaosema kuwa na serikali tatu kutaua Muungano, huenda ni kweli lakini kama msingi mkuu wa kuchagua idadi ya serikali ni kuulinda Muungano basi suluhisho ni kuwa na serikali moja.
Nasema hivyo kwani hizi mbili za sasa zimetumika nguvu nyingi na hata wakati mwingine unaweza kusema hila, ulaghai au mabavu ili kuzifanye ziwepo huku tuendako hazitatufaa.
Nasema hivyo kwani hizi mbili za sasa zimetumika nguvu nyingi na hata wakati mwingine unaweza kusema hila, ulaghai au mabavu ili kuzifanye ziwepo huku tuendako hazitatufaa.