Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jibu ni kwamba wote wapigwe faini, we huwajui watanzania walivyo na viherehere, wanajifanya wana haraka sijui haraka ya kwenda wapi. Mtu anaona gari imejaa analazimisha kuingia halafu anataka umsaidie kumbebea begi au mtoto. Bado akukanyage na ole wako umsemeshe majibu yake utaendelea kuyatafakari wiki nzima. PIGA FAINI ISIYOPUNGUA 50,000/ ABIRI PAMOJA NA WENYE GARI yaani dereva na konda. Nchi gani ya hovyo haistaarabiki km hii, ni aibu majirani wanatushanga na kutudharauYaani kuishi nchi hii ya Tanzania imekuwa nongwa sana, kila eneo wafanyabishara wanajiamlia kufanya yao.
Waendesha daladala wanapakia abilia hadi mlangoni, watu wanasimamiahwa na kupangwa kama magunia ya mikaa.
Kwani serikali hatuwezi kufanya hata hili la usafiri kwa kuzingatia level seat nchi zingine zikaja kujifunza hapa kwetu Tanzania?
Cha kufanya serikali toa tamko kwa nchi nzima hakuna abiria kusimama kwenye chombo cha usafiri hasa daladala maana najua angalau kwenye vyombo vingine vya usafiri wa masafa marefu wanazingatia level seat.
Yaani mimi huwa nashangaa Trafiki wa Tanzania anasimamisha gari ndogo mfano Harrier au Juke nakuanza kuizunguka zunguka kukagua huku akiiacha daladala inampita mbele yake ikiwa imejaza abiria hadi mlangoni na ilhali wakijua hiki ni kichume na sheria za usafirishaji.
Serikali toa tamko kwamba Trafiki ashushe abiria yoyote aliyepanda daladala kwa kusimama, hiyo ndiyo iwe adhabu yake huku konda na dereva walioruhusu abiria kusimamia kwenye gari yao wakipigwa faini ya Tshs 30000.
Hii itasababisha abiria, konda na madereva kuheshimu sheria na usalama barabarani.
Hivi kwa ujazaji wa abiria wakiwa wamesimama hadi milangoni, tulishajiuliza endapo daladala hiyo inapata ajali hivi hao abiria walio simama watakuwa na hali gani? Au ndo kusema serikali itakuja na salam za pole kwa wananchi walioondokewa na wao.
Lakini pia serikali kupitia mkurugenzi wa halmashauri waone umuhimu wa kuwapunguzia tozo haya magari yanatoa huduma za daladala kwa wananchi wa Tanzania kwa sababu inawezekana wanajaza ivyo abiria ili wapate pesa za kulipa kodi za TRA na Tozo za halmashauri.
Lakini pia serikali ione umuhimu wa kupunguza kodi za forodha za uingizaji magari ya abiria ili wawekezaji waingize magari mengi ya abiria kwa ajili ya ku_accomodate the excess supply ya abiria inayochangiwa sana na ukuaji wa miji yetu na uzalianaji mkubwa kunakopelekea uongezekaji mkubwa wa idadi ya watu Tanzania.
Wazo zuri mkuu, lakini angalia study hizi mbili walifanya wenzetu.Nunua usafiri wako kuepuka mlundikano.
Kule ni ulaya hapa ni Africa,mbingu na ardhi azifanani.Wazo zuri mkuu, lakini angalia study hizi mbili walifanya wenzetu.
View attachment 2896961
View attachment 2896962
Unaona public transport moja (mfano M/Kasi) inavyoweza kupunguza private cars nyingi mjini? Kwahiyo itapunguza foreni, hewa ya ukaa, joto, ajali zisio maana, kwahiyo itaongeza efficiency.
Sema ndio ivo still wazo lako kwa sasa hamna jinsi zaidi ya kujipiga kununua tu gari.
Ila wizara husika wangekomaa hapa kuweka sera nzuri ya usafiri. Watu wanajaa hadi mlangoni kwasababu magari machache hawana option.
Acha tu man. Ili bara kuishi balaa.Kule ni ulaya hapa ni Africa,mbingu na ardhi azifanani.
Hivi unajua kwamba tabia hutengenezwa?Mengine huwa mnaongea tu kwakua mnapenda lawama, nchi zilizoendelea zenyewe kwenye treni zao nyomi lipo kama kawa.
Abiria hulazimishwi kupanda, konda hakubebi upande gari yake.
Usafiri sio gari tu hata baiskeli ni usafiri wenye kuimarisha na afya.Wazo zuri mkuu, lakini angalia study hizi mbili walifanya wenzetu.
View attachment 2896961
View attachment 2896962
Unaona public transport moja (mfano M/Kasi) inavyoweza kupunguza private cars nyingi mjini? Kwahiyo itapunguza foreni, hewa ya ukaa, joto, ajali zisio maana, kwahiyo itaongeza efficiency.
Sema ndio ivo still wazo lako kwa sasa hamna jinsi zaidi ya kujipiga kununua tu gari.
Ila wizara husika wangekomaa hapa kuweka sera nzuri ya usafiri. Watu wanajaa hadi mlangoni kwasababu magari machache hawana option.
NajuaHivi unajua kwamba tabia hutengenezwa?