Serikali piga marufuku mrundikano wa abiria kwenye Daladala

Jibu ni kwamba wote wapigwe faini, we huwajui watanzania walivyo na viherehere, wanajifanya wana haraka sijui haraka ya kwenda wapi. Mtu anaona gari imejaa analazimisha kuingia halafu anataka umsaidie kumbebea begi au mtoto. Bado akukanyage na ole wako umsemeshe majibu yake utaendelea kuyatafakari wiki nzima. PIGA FAINI ISIYOPUNGUA 50,000/ ABIRI PAMOJA NA WENYE GARI yaani dereva na konda. Nchi gani ya hovyo haistaarabiki km hii, ni aibu majirani wanatushanga na kutudharau
 
Nunua usafiri wako kuepuka mlundikano.
Wazo zuri mkuu, lakini angalia study hizi mbili walifanya wenzetu.





Unaona public transport moja (mfano M/Kasi) inavyoweza kupunguza private cars nyingi mjini? Kwahiyo itapunguza foreni, hewa ya ukaa, joto, ajali zisio maana, kwahiyo itaongeza efficiency.

Sema ndio ivo still wazo lako kwa sasa hamna jinsi zaidi ya kujipiga kununua tu gari.

Ila wizara husika wangekomaa hapa kuweka sera nzuri ya usafiri. Watu wanajaa hadi mlangoni kwasababu magari machache hawana option.
 
Kule ni ulaya hapa ni Africa,mbingu na ardhi azifanani.
 
Serikali haina muda huo
 
Mengine huwa mnaongea tu kwakua mnapenda lawama, nchi zilizoendelea zenyewe kwenye treni zao nyomi lipo kama kawa.

Abiria hulazimishwi kupanda, konda hakubebi upande gari yake.
 
Nakumbuka enzi za Mwaibula hali ilikuwa ni nzuri sana, jamaa daladala zote zilikuwa zinamheshimu na huduma ilikuwa bora sana
 
Mengine huwa mnaongea tu kwakua mnapenda lawama, nchi zilizoendelea zenyewe kwenye treni zao nyomi lipo kama kawa.

Abiria hulazimishwi kupanda, konda hakubebi upande gari yake.
Hivi unajua kwamba tabia hutengenezwa?
 
Usafiri sio gari tu hata baiskeli ni usafiri wenye kuimarisha na afya.

Kule Nairobi watu wanajigawa kwenye utumiaji wa usafiri, wengine wanatembea kwa miguu ili kukwepa foleni na kupunguza mlundikano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…