Serikali pitieni upya Sera ya 'Elimu Bure', ikiwezekana ifutwe kabisa

Mkuu,

Usilete mawazo mfu kwenye jukwaa la JF utaghadjabisha wengi labda kama ni watetezi wa umwinyi na ubwanyenye kwamba waliokuwa nacho ndio wapate elimu kisha waje wawatawale wajinga hili haliwezekani kwa sasa.

Kwanza wigo wa kuto elimu bila malipo ya ada unatakiwa upanuliwe hadi kidato cha sita, vyuo vyote vya kati huku vyuo vikuu wanafunzi wote wanaochaguliwa kujiunga wapewe mikopo sawia kwa asilimia 90% hadi 100% na marejesho baada ya kumaliza upungzwe had asilimia 8% badakla ya asilimia 15% inavyofanyika kwa sasa..

Inavyoonesha wewe unamgongano wa maslahi kwamba unapata ushindani mkubwa na huna uwezo kujipangia ada ba malipo mengine yanayoumiza jwassiokuwa nacho.

Wananchi hawataki mawazo yako ya kibinafsi yaliyolenga kuimarisha biashara yako ya uendeshaji wa shule au taasisi za utoaji elimu kwa gharama kubwa yenye kuleta faida badala ya kuwa ni huduma.
 
Mtoto wa mwanasiasa gani anasoma huko? Ukitaka mwanao awe ganja man mpeleke uko
 
Kumbe huko kwenu bado kuna elimu bure?!
Sisi huku wazazi wametangaziwa mchango wa kila mzazi pesa ya kujenga madarasa, vyoo vya waalimu na wamepewa week moja kila mzazi awe amemaliza kulipa vinginevyo mtoto wako akitoka likizo aje na mazazi.!
Sasa hapo kuna elimu ya bure tena?
 
Ndugu,
1. Watoto kufeli masomo ya sayansi hiyo imekuwepo tangia zamani, hawajawahi kufaulu, sasa elimu bure imehusikaje?
2. Hela ya vifaa vya maabara hupelekwa mashuleni kila mwezi, kama shule hazinunui mkawaulize pesa wanapeleka wapi.

3. Changamoto ya madawati ipo tu maana kila mwaka wanafunzi wanaongezeka.

4. Kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi ni jukumu la mzazi na ni wajibu wake, wazazi wakishindwa sio kosa la serikali, ni uzembe wao.
 
Wazaz wktoa pesa wnkua wachungu na pesa hvo hufatilia mwenendo w mtoto saiz hkuna mweny hbr hiyo kw sbb ya elimu bure

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Critical thinking,big up.
 
Haya majibu ni mepesi sana.Kwa hiyo hakuna umhimu wa kuongeza ufaulu kwenye masomo ya sayansi,na pia kuondoa uhaba wa madawati???? What's this!!!
 
No retreat no surrender huyo ndio big boss
 
So sera ya chadema ilikuwa changa la macho
 
Walikurupika, hawakujiandaa kikamilfu kutekeleza hii sera.
Unaikana sera yako na lowasa wako .huna akili kabisa kama umeanza kikengeuka wazo la kusema jpm anatekeleza ilani yenu imeishia wap
 
Haya majibu ni mepesi sana.Kwa hiyo hakuna umhimu wa kuongeza ufaulu kwenye masomo ya sayansi,na pia kuondoa uhaba wa madawati???? What's this!!!
Soma mada vizuri na uangalie nilichojibu, acha kukurupuka.
 
No retreat no surrender huyo ndio big boss
Kikwete alijaribu kwa kufuta ada za mitihani ya kidato cha pili na nne lakini alivyoona serikali inaingia gharama kubwa aliamua kufuta huo mpango. Naamini hata huu mpango utafutwa tu kama sio kipindi hiki basi kipindi kijacho.
 
Njoo na Statistical evidence za kabla ya elimu bila malipo na baada ya elimu bila malipo kwa kila changamoto uliyotaja hapo juu ili tuweze kuamini ulichoandika, tofauti na hapo tutajua umetumwa na chadema. provide statistical facts za before and after na utoe statistical proof by using any statistical test kama tunaweza kukubaliana na ushauri wako.
 
Wazo zuri.Tatizo ni mapokeo.Je,wenye mamlaka watasikiliza????
Tangu "Elimu bure" ianzishwe(kinadharia)",imekuwa mtaji kisiasa.Sidhani kama watakubali kuupoteza.

Pia si kweli kuwa elimu ni bure kwani tuna watoto katika shule tofauti na kila shule ina taratibu za michango ambayo ukijumlisha kwa mwaka ni zaidi ya karo ya 20,000 na 70,000 !(shule za serikali.

Na kuwa siasa kutawala nyanja zingine(utaalamu/taaluma) ndiyo chimbuko la mapungufu yote haya.Unakuta Mkuu wa Wilaya/Mkoa anaagiza kukamatwa na kuwekwa mahabusu "mtendaji" kwa tuhuma (ambazo hazijathibitishwa) na hivyo kushusha ari ya kazi na ubunifu. Tangu mtindo huu utamalaki sijasikia yeyote aliyewahi kutumbuliwa na DC/RC kachukuliwa hatua zaidi kwa maovu aliyotenda.(Niko radhi kukosolewa).

Itoshe kusema kuwa ili tusonge mbele,mifumo mbali mbali inayoongoza Taifa letu ibadilishwe.Kwa kuanza na mitaala ya Elimu,uendeshaji wa Taasisi za Elimu,Utawala/siasa kutoingilia(bila sababu za msingi), kuheshimu taaluma na mipaka ya kazi na jamii kufunguka.
 
Kwakuwa watotowako na ndugu zako wrote wanasomea shule za kishua, ndio maana umeona shule wañazosomeshea wenyekipato kidogo nazo wasome kwa kulipia kwakuwa wewe na familia yako mnaweza kumduuu. Mkifanikiwa kifedha mbona mbona mjisahau kana kwamba mlizaliwa nazooo?? Kumbuka ulikotoka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…