TISS kweli ina meno kwa watu masikini na wasiokuwa na nguvu za kimamlaka na pesa ila kwa wenye pesa na wenye mamlaka ya juu wanakuwa vibogoyo kabisa.
Pamoja na TISS kuna na nguvu kwa normal people na ubogazi wao still kumuua mtoto wa huyo mbarikiwa ni kitu kisichowezekana hata kama wangekuwa bogazi vipi, wanamuua kwa lipi na point ya kumuua ni ipi ? Huyo mbarikiwa ana impact gani nchi hii zaidi ya waumini wake wasiofika hata 200. TISS waache kumuua huyu mbarikiwa waende wakaue mtoto innocent [emoji38] lengo ni nini kwamba wameshindwa kumuua mlengwa mwenyewe ? Mtoto wa mbarikiwa amekufa lini ? Na Masoro amepata u DGIS lini? Hata kama alikuwa deputy na director wa internal affair still hakuna mashiko ya kufanya ivyo. Mtoto amekufa August 2022 , huyo Masoro kawa DGIS 2023 [emoji38].
Huyo mbarikiwa kinachomsubua ni Afya ya Akili tena ukichanganya na dini ndo kabisa matokeo yake haya kusema mtoto ameuliwa , kila fallacy inayokuja kichwani mwake basi anaichukulia kama maono au kitu halisi.
Uzuri haya mambo ya imani yanakinga watu wasionekane machizi , maana imani unaweza ukaamini chochote kile ilimradi ni kitu kisicho na uthibitisho ndo maana kuna yule nan sijui ana id ya kieebrania (mwalimu) na wenzake wanatuambia Tanganyika ndipo Eden mpaka mambo ya vitabu vya isaya wanasema ni utabiri kuhusu Tanganyika [emoji23][emoji23].
Huyo mbarikiwa hana tofauti na kina Mackenzie.
Huwezi kujua kwa sababu wewe na yeye (Mch Mbarikiwa) mnaishi ktk frequency za ulimwengu tofauti kabisa.
Kwa macho yako unamwona kama hana impact yoyote iwe kumuulia mtoto wake au kumuua yeye mwenyewe, lakini wenzio hao waabudu miungu wanajua impact yake na wanajua wanachokifanya na sababu yake.
Hapo ni falme mbili zinazopambana. Ufalme wa uovu na maovu vs ufalme wa NURU na HAKI.
Mungu hutumia wanaonekana wanyonge, kapuku, waliodharaulika na kutwezwa ili kudhihirisha nguvu na uwezo wake ktk ulimwengu huu kwa kusudi la kuwaaibisha wanaojiona wenye nguvu na bora.
Rejea tukio la wakoma wanne lililo rekodiwa kwenye biblia yako ktk kitabu cha
2 Wafalme sura ya 7 yote na ili kupata mantiki vizuri anzia sura ya 5, 6 na ingia hiyo ya 7.
Wakoma ni watu waliokuwa wanyonge sana na kutengwa na jamii yote. Hata hivyo, Mungu aliamua kuwatumia hao hao ili kuikoa nchi yote ya Samaria iliyokuwa kwenye changamoto ngumu za kiuchumi na njaa tokana na vita na nchi jirani yao ya Waaramu au Washami.
Kabla ya hapo wenye hekima ya kidunia, wasomi wa udaktari na uprofesa wa nchi ya Samaria walishatumia kila aina ya ujuzi na maarifa na hekima yao waliyoipata darasani kutafuta majibu ya changamoto hizo bila mafanikio.
Lakini Mungu akapitia kwa wakoma wale wanne waliokuwa wanadharaulika na kila mtu na kuikoa nchi yote na kuwakimbiza maadui wao - jeshi la Washami na kuondoka kabisa kwenye nchi yao. Nchi ya Samaria ikapona.
Kwa hiyo, Mungu anaweza kutumia kitu kinyonge kabisa kuleta muujiza. Acha dharau na kama hujui au huna la kusema, hekima ikuongoze kunyamaza kimya.
Nakuhakikishia jambo moja kuwa, kupitia Mch Mbarikiwa Mwakipesile, jambo kubwa linakwenda kutokea nchi hii na hapo ndipo utakapokiri kwa kinywa chako kusema; "..loooh, kumbe huyu ni mtu wa Mungu wa kweli."