Serikali, punguza kodi ya Sukari sio Pombe

Magendo hata Kwenye pombe yapo TU, watu wanabwia viroba Kama kawaida
 
Sukari haifai,

Sukari inasababisha magonjwa,Ukiugua kisukari
1. Utapoteza Nguvu za kiume
2. Utakaribisha shinikizo la damu..
Unavyotetea upuuzi kwa nguvu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndio maana mwisho wa siku wabunge Kama wakina Msukuma huwa dharau wazi wazi kabisa
 
Aisee usifananishe pombe na vitu vya kijinga tafadhali sana [emoji2]

Sukari Ina siasa yake kama madini na kuna watu wameikamata vizuri hata Magu alishindwa Ile vita akaishia kusema watu wanahodhi sukari Ila hajakamata hata mtu mmoja...
Kweli kabisa Mwendazake alijaribu kugusa hii biashara akaishindwa, mwisho wa siku akaamua kumpa Bakhresa mashamba bure ili kupunguza nguvu ya hao watu.
 
Bajeti ilipita kwenye baraza la mawaziri hata maza alikuwa mwenyekiti
 
Kwa uelewa wangu,ni kwamba ukiona Nchi imeshusha sana kodi kwenye pombe wakati uchumi wake bado upo chini ( kumbuka Tanzania ipo uchumi wa kati wa chini), basi tambua hatua hiyo imechukuliwa kuwafariji kundi kubwa ambalo hawana kitu, njia hii aliitumia sana mkoloni kuwafariji wafanyakazi husasani askari ambao mishahara ilikuwa midogo, kipindi hicho pombe iliuzwa bei ya chini sana. Askari wengi walifarijika na kujiburudisha huku wakisahau madai mengi ya msingi.

Pombe sijui ina nini! hapa naongea na kwa uzoefu,angalia hata kwenye sherehe watu wapo radhi wakose chakula sio pombe, chakula hata kiwe kibaya watu hawatauliza ikiwa tu monde itakuwepo ya kutosha. watawala nao wanajua nguvu ya hii kitu. Subiri baada ya bei ya pombe kushuka mwaka huu kama utaona kelele juu ya bei za bidhaa muhimu kama sukari n.k, nakuhakikishia pombe ikishushwa labda kwa kuuzwa shilingi 1000 kwa chupa na bei ya sukari ikapanda kwa 1000 zaidi, wanywaji wa pombe ambao ni wengi watanyamaza kama hilo haliwahusu.

Mwisho namalizia " watu wanywe bia, kwa maana bia ni uchumi"- Chalamila.
 
Kweli yaani Mwigulu ana maajabu eti hiyo ndio njia ya kuhimiza matumizi ya shairi inayolimwa ndani ya nchi.

Hivi huyu Waziri huwa anakaa hata na wadau wa sekta mbalimbali kuwasikiliza Ili kujua wapi pa ku adjust?
 
Mleta mada inaonekana unatabia ya kutongoza huku unamkandia mshikaji mwingine kwani unashindwa kutetea hoja ya sukari bila kutaja gambeee?!!!!
 
Imagine castle lite moja 1500 halafu 1kg ya sukari 3000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…