Serikali, punguza kodi ya Sukari sio Pombe

kuna mtu anakunywa castle moja?
Kwani sukari familia inatumia kilo moja tu?

Mimi ni mlevi sana but pombe ni starehe inatakiwa iongozewe kodi tunywe kwa kujiamini kifua mbele

Maana tutakuwa walipa kodi wazuri
 
Kwa nini wasiongeze kodi kwenye pombe tuwanusuru vijana wanaoangukia kwenye ulevi wa kupindukia na kutelekeza familia zao na wengine kufa kwa kuzidisha kilevi, naliongea hili kwa uchungu kwani vijana siku hizi wanafanya mashindano ya kunywa pombe kali bila kujali wamekula chakula vizuri na hali ya kiafya ya viungo muhimu kama ini na figo, matokeo yake wengine wanakufa ghafla kwenye ulevi..........serikali wekeni kodi kubwa hasa kwenye vilevi vikali.
 
Kwani sukari familia inatumia kilo moja tu?

Mimi ni mlevi sana but pombe ni starehe inatakiwa iongozewe kodi tunywe kwa kujiamini kifua mbele

Maana tutakuwa walipa kodi wazuri
familia yako inatumia kg moja per day?

kama ni hivyo soon mtabeba maradhi
 
Kama kupandisha kodi kwenye pombe ingewafanya watu kuacha wangeisha acha siku nyingi sana!!lakini bado wapo vile vile, sana sana wataingia kwenye pombe halamu tu, ambazo hata kodi hazitozwi!!kwenye uchumi wa nchi sukari ya majumbani haina tija sana, zaidi ni kisiasa, kulinganinisha na sukari ya viwandani ndio maana hata bajeti hii imepunguziwa sana kodi, kwani ina matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi, na hata hiyo kodi ya vileo vinavyotengenezwa ndani , inavyotumia shaili ni kuwasaidia pia wakulima., na hata hivyo usitegemee kuona badiriko sana la bei kwani kodi inapunguzwa huku, inaongezwa kule!!
 
Ki uchumi huwezi kimbilia tu kuongeza kodi kwenye baadhi ya bidhaa(za anasa)ambazo kwa kiasi kikubwa ndipo unategemea mapato makubwa huko!!miaka yote kwenye pombe , kamali ndipo kuna mapato makubwa sana , sasa useme mzigo wote wa kodi uuweke huko, ili sehemu nyingine zipate nafuu, huku nako pa ki fail hata huko kwenye kilimo hakuna kitakachoendelea!!kwenye kupandisha kodi ya bidhaa kuna vitu vingi vya kuzingatia.Nchi hii ukisema kweli unataka kuinua kilimo inavyotakiwa lazima sekta nyingi zisimamame kwanza, KUPANGA NI KUCHAGUA.
 
Ongeza na lile la wastaafu; eti Mama amesikia kilio chao cha fedha zao kukopwa na serikali na hivyo kutolipwa mafao yao - suluhu yake - serikali itageuza hayo madeni kuwa hati fungani za serikali (yaani aina nyingine ya deni la serikali), Halafu anamalizia eti hiyo inaenda kumaliza tatizo - shame/aibu tupu

Unganisha na la kodi za majengo!! Eti shs 1,000 kwa mweiz kwa kila mita, Je hajui kuwa sheria haitozi kodi kwa majengo ya wazee wa umri wa kuanzia miaka 60 kwenda mbele, Je hao wana mita tofauti?
 
Wanywa Pombe bei gani sasa kwa chupa
 

Sukari haifai kwa matajiri wanaoishi “kizembe”; lakini ni muhimu kwa wanyonge wengi wanaochakarika mashambani, migodini na mitaani. Wafikiriwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…