Kama tukitumia akili ya kulalamika basi kila siku kazi iitakuwa nikuwasihi na kuwaomba serikali watusaidie kutatua kero ya ajira ile hali serikali yenyewe inaendeshwa na watu kama wewe na mimi.
Hebu tazama juzi tu akina mama lwakatale walikuwa hapo bungeni, leo hadi akina babu tale na Mwanafa sasa hivi wapo bungeni.
Sasa tukiendelea na huu utaratibu tusubirie akina shilole Joyce kiria, steve nyerere, akina kingwendu na akina swebe ndio wakawe wabunge wetu kutuongelea.
Nachotaka kusema ni kuwa kada ya vijana wa kisasa hatupo serious na maisha yetu. These so called leaders, kama kweli ni leaders then they are leading fools. Sababu only a fool leader will lead fools.
Madhara hatuwezi yaona sasa, but in the next 30 to 40 years from now. Retirement age ikifika. Tutakapokuwa wazee wa miaka 50+ tukiitafuta 60, 70, 80 na 90 kama huo mwili utaruhusu ndipo tutaona gharama ya kucheka na hawa jamaa wanaojiia politicians kwenye shughuli zetu za maendeleo.
Kwasasa tuendelee kuwachekea wakati wanachezea pesa zetu vile wanavyojiskia. Wakati mkilalamika kukosa ajira na vipato, wenzenu kodi inayokusanywa plus misaada wanayopewa kupitia jina la nchi na pia wanapouza na kuweka rehani rasilimali zetu kwa visingizio vya kututafutia maisha bora, tazama wao wanaishi vipi?! Kuanzia wapinzani na chama tawala. Tazama wanavyomumunya pesa zetu kama vile ubuyu wa zanzibar huku wakitufariji kinafiki.
Hebu fuatilia mishahara ya viongozi wote kuanzia rais, mawaziri na manaibu wao, makatibu wizara etc, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, halafu ujiulize je na wao wanavumilia shida au kuishi kwa matumaini?!
Siku wananchi, especially kada ya wasomi, tutakapoanza kuhoji matumizi ya pesa zetu every single senti inayokusanywa na serikali kuwa inakwenda wapi then it's the day tutaanza kupiga hatua kumaliza mjadala juu ya ajira. Kimya chenu kutohoji ndicho kinachofanya jamaa kuwa na ujasiri wa kukaa kimya na kukaushia issue ya kukosekana ajira.