Serikali: Simamieni shule binafsi.

Serikali: Simamieni shule binafsi.

Same ORG

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
321
Reaction score
21
Nipo hapa tz nimempeleka mtoto wangu shule inaitwa Yemen ipo hapa Dar, shule ambayo unalipia sh.milioni moja kwa mwaka kwa primary.mtoto wangu Alifanya interview na akapasi vizur lakini cha kushangaza baada ya kuanza class mwalimu wake akaniambia mtoto wako hafahamu kabisa itabidi umuanzishe tuition.

Mimi kwa mshangao mkubwa nikajiuliza ilikua na haja gani mtoto wangu kumpeleka shule ya pesa? Ninajua maana ya kutoa pesa na ukailipa shule ni kufundishwa mtoto vizuri na sio kufanywa biashara nyengine ya tuiotion ndani yake. Hii ni biashara ndani ya biashara, iv kweli hapa elimu ipo au nimepoteza hela yangu?kwanini shule ya pesa iendeshe tuition ndani yake au walimu hawapati mshahara wao kama kawaida? Ni jambo la kushangaza. Je na kama mtoto wangu atakua hasomi hii tuiotion anayoitaka mwalimu ndio itakua nimepoteza hela yanguna atakua hawezi kufaulu chochote?hapa nimeanza kupatwa na waswas mkubwa sana, na sidhani kwamba wanataka asome tuiotion kwa kumuongeza juhudi isipokua ni biashara tuu.

My take: Serikali iunde kamati ambayo iwe ya kila mwaka kwakua ikiwa ni ya kudumu inaweza ikatawaliwa na rushwa.kusimamia shule zote za binafsi kuanzia kuyakagua masomo,nidhamu,mazingira ya shule,serikali itathmini masomo yale kuanzia nasery,primary,secondary mpaka vyuo.
Baada ya tathimini itoe beii kutokana na elimu,nidhamu na mazingira ya shule husika.
 
Shule ya ada ya tzs 1,000,000 sio ya pesa tena baba (average 330,000 kwa term na wana term tatu). Hiyo ni st kayumba ya academia. Nakushauri jumatatu uende ukakae darasani usikilize mwalimu anapokuwa anamfundisha mwanao kingereza kibovu afu urudi tukushauri.

Hiyo shule ya Yemen wapi? Samahani lakini.
 
Wakisimamia Mulugo atakosa biashara nae ana shule zake
 
Shule ya ada ya tzs 1,000,000 sio ya pesa tena baba (average 330,000 kwa term na wana term tatu). Hiyo ni st kayumba ya academia. Nakushauri jumatatu uende ukakae darasani usikilize mwalimu anapokuwa anamfundisha mwanao kingereza kibovu afu urudi tukushauri.

Hiyo shule ya Yemen wapi? Samahani lakini.

Mzee wangu elimu sio pesa, kama elimu ni pesa nchi za uarabuni zingelikua juu sana saivi, ndio maana hapa nimesema pesa yoyote inayolipwa sasa inahitaji usimamizi kwakua naamini hata wanaolipa milioni 8 kwa mwaka nao wanafeli na wazee wao wanasikitika.
 
Jenga tabia ya kukagua majina ya vitu, kuna ka-ukweli kwenye hili. Juzi nilienda kununua wembe nikaambiwa zipo nyembe zinazoitwa Al-shabab! Ilibidi niende sehemu nyingine. Sasa ndugu yangu shule inaitwa Steven Mwenyehasira huna wasiwasi na jina?
 
Shule zingine hazina management nzuri kwa sababu shule ambayo ina mazingira mazuri,walimu wazuri na mambo mengine yanayotakiwa ili shule iitwe shule sioni kama kuna umuhimu wa mtoto kusoma tuition,tuition mashuleni haziruhusiwi japo sijui kifungu chochote cha sheria kinachokataza tuition cha msingi chukua hatua za kufuatilia kama kinachofundishwa hapo kinaendana na uhalisia wa gharama unazotoa kisha ukisharidhika au kama hujaridhika mhamishe mwanao mabona kuna shule nzuri saana kwa kiasi hiko cha pesa.
 
Back
Top Bottom